Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Bwana Mustapha Aboud Jumbe (kushoto) na Mtendaji mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba (kulia) wakitia saini
nyaraka ya Makabidhiano ya Vituo vya TEHAMA vilivyojengwa na UCSAF,
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula
(katikati) akishuhudia
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (katikati) akikabidhi nyaraka
zilizosainiwa za makabidhiano ya Vituo vya TEHAMA kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ) Bwana Mustapha Aboud Jumbe (kushoto) , (kulia) ni na
Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina
Mashiba akushuhudia
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (katikati) akikabidhi funguo
za Vituo 10 vya TEHAMA kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ) Bwana Mustapha Aboud Jumbe (kushoto) , (kulia) ni na Mtendaji
mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba
akushuhudia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ) Bwana Mustapha Aboud Jumbe (kushoto) akionesha bahasha yenye
funguo za Vituo 10 vya TEHAMA mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (katikati), (kulia)
ni na Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi.
Justina Mashiba
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ) Bwana Mustapha Aboud Jumbe (kushoto) akionesha bahasha yenye
funguo za Vituo 10 vya TEHAMA mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (kulia)
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
ndugu Mustapha Aboud Jumbe (wa kwanza kulia) akikagua ufanyaji kazi wa
vifaa vya TEHAMA mara baada ya makabidhino (kulia kwake) ni Katibu Mkuu
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (wa pili kulia waliokaa) akiwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Bwana Mustapha Aboud Jumbe (wa
pili kushoto waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi na
Watendaji wakuu wa Taasisi na Wizara wa Sekta ya Mawasiliano kutoka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,
(kushoto waliokaa) ni Dkt. Jim Yonazi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Zainabu Chaula (wa pili kulia waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano
na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Bwana Mustapha
Aboud Jumbe (wa pili kushoto waliokaa) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jim Yonazi (kushoto waliokaa) wengine ni
Wakurugenzi na Watendaji wa Taasisi na Wizara wa Sekta ya Mawasiliano
kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar
…………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Zainabu Chaula amekabidhi vituo 10 vya TEHAMA kwa
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Bwana Mustapha
Aboud Jumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kuagiza vituo
hivyo vitumike kuwapatia wananchi wa Zanzibar huduma za TEHAMA hasa wale
ambao hawana namna ya kupata huduma hiyo
Vituo hivyo vilivyojengwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote (UCSAF) kwa gharama ya shilingi 1,138,000,000 vimekabidhiwa
rasmi katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katikati ya wiki
kisiwani Unguja katika Mkoa wa Mjini Magharibi eneo la Kiembe Samaki
“Vituo hivi vitumike kuongeza
tija na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa
Zanzibar,kwa kutambua hilo Wizara yenye dhamana ya mawasiliano inapaswa
kuandaa mwongozo wa utendaji kazi ili vituo hivi viweze kujiendesha
vyenyewe na hatimaye kuwezesha ujenzi wa vituo vingine kama hivi angalau
kituo kimoja kwa mwaka”, alisisitiza Dkt. Chaula
Naye Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Bwana Mustapha Aboud Jumbe amesema
kuwa ujenzi wa vituo vya TEHAMA Zanzibar ni jambo linaloimarisha
Muungano kwa kuwekeza moja kwa moja kwa wananchi na kuzitaka taasisi
nyingine za Muungano kutafuta mbinu za kuwasogezea huduma wananchi.
“Maisha ya siku hizi yamekuwa ya
kidijitali ambapo huduma nyingi zinafanyika kwa mtandao kama vile fomu
za maombi ya ajira, passport na viza zinajazwa mtandaoni, hivyo
kusogeza huduma hii kwa wilaya zote 10 ni jambo muhimu sana”, alisema
Bwana Jumbe
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) Bi. Justina Mashiba amesema kuwa
matarajio baada ya ujenzi wa vituo hivyo ni kuamsha ari ya matumizi ya
TEHAMA kwa wananchi wote wa maeneo husika wenye nia ya kutumia huduma ya
hiyo pasipo kubaguliwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Vituo vya TEHAMA
katika mikoa yote kumi Zanzibar ambapo kisiwani Unguja Vituo vimejengwa
katika mikoa Sita ya kusini magharibi-Tunguu, Mjini
Magharibi-Mwera,Kusini Unguja-kitogani, Kaskazini Unguja-Mkokotoni,Mjini
Magharibi-Kiembe Samaki ,kaskazini unguja-Mahonda na Kisiwani Pemba
Vimejengwa katika eneo la Wete, macho manne,Micheweni na Chonza, kwa
lengo la kuwasogezea wananchi huduma za TEHAMA.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
No comments :
Post a Comment