Wawekezaji
wa ndani ya nchi wamehamasishwa kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa
viwanda vya mbolea hapa nchini ili kusaidia upatikanaji wa mbolea bora
na yenye gharama nafuu kwa wakulima.
Katibu
Mkuu wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa wito huo jana (11.07.2020)
wakati wa ziara yake ya kikazi wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa
kujionea hali ya uzalishaji mazao ya pareto na chai.
Kusaya
alisema kuwa hali ya uzalishaji mazao hayo umekuwa ikishuka mwaka hadi
mwaka kutokana na malalamiko ya wakulima kushindwa kumudu gharama ya bei
kubwa ya pembejeo na mbolea.
“Nitafurahi
zaidi nikisikia watanzania wanaanzisha uwekezaji katika viwanda vya
mbolea ili tusaidie wakulima wetu kwani kwa sasa katika baadhi ya maeneo
wakulima wengi wanashindwa kununua mbolea mfuko wa kilo 50 kwa shilingi
90,000 “ alisema Kusaya
Akiwa
kijiji cha Mkonge wilaya ya Mufindi Katibu Mkuu huyo alipokea
malalamiko ya wakulima wadogo wa chai kuwa chai yao inakataliwa na wenye
viwanda kwa madai kuwa ina ubora mdogo uliosababishwa na kutumia mbolea
yenye ubora mdogo .
Wakulima
hao wa chama cha ushirika cha wakulima wa chai Mkonge wanadai
kukopeshwa mbolea na kampuni ya Uniliver ya Mufindi ambayo pia ni mmoja
wa wanunuzi wanaokataa kununua majani mabichi ya wakulima hao na
kusababisha hasara kwa wakulima.
“
Chai tulipeleka mwaka huu kiwandani Uniliver tukaambiwa haina ubora
kisha wakaimwaga kwa kuwa tulitumia mbolea ya minjingu isiyo na
ubora,hii hasara nani atatulipa “ alisema Jimson Sigala mkulima wa chai
Katibu
Mkuu huyo aliongeza kusema wizara ya kilimo inahitaji mkulima atumie
mbolea itakayoongeza tija katika uzalishaji hivyo amewasihi watanzania
kujitokeza kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda ndani ya nchi na kuwa
serikali ya Awamu ya tano itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji.
Kwa
mujibu wa Wakala wa Udhibiti wa Mbolea (TFRA) hali ya upatikanaji wa
mbolea nchini imeongezeka kutoka tani 302,482 mwaka 2015/2016 hadi tani
604,978 mwaka 2019/2020 hata hivyo mahitaji bado ni makubwa sana kwani
mbolea nyingi zinaagizwa nje ya nchi na kuwa bei kubwa.
Katika
hatua nyingine Katibu Mkuu Kusaya amewasihi wakulima wa chai Mufindi na
kote nchini kutumia Kituo cha Utafiti wa zao la Chai ( TRIT) kupata
huduma za ushauri ili waongeze tija katika uzalishaji wa zao la chai
nchini.
“
Wakulima nendeni kwenye kituo chetu cha Utafiti TRIT kupata elimu juu
ya kilimo cha chai ikiwemo kupata huduma ya upimaji afya ya udongo kujua
aina ya virutubishi na mbolea inayotakiwa kuongeza uzalishaji na
kuwezesha mkulima anufaike na kilimo” Kusaya alisisitiza
Wakulima
wadogo wa chai Mufindi waliomba serikali iwasaidie kupata bei nzuri ya
chai kwani bei ya sasa ni ndogo na haiendani na gharama za uzalishaji.
Akizungumza
kwa niaba ya wakulima Abeid Mhongole mkazi wa Luhunga Mufindi alisema
bei ya shilingi 314 kwa kilo moja ya majani ya chai haileti manufaa kwa
wakulima na zaidi inawakatisha tamaa kuendelea kuzalisha zao la chai.
Akijibu
kero hiyo Katibu Mkuu Kusaya alisema atakutana na Katibu Mkuu wizara ya
Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe hivi karibuni kujadili namna ya
kupata ufumbuzi wa malalamiko ya bei ya zao la chai na kuwa ikibidi
wasaidie kupatikana kiwanda cha chai kwa wakulima wadogo.
Aidha
Kusaya aliwataka viongozi wa chama hicho cha ushirika kuwasilisha
maombi yao ya kupta mtaji katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ili
waweze kupata uwezo wa kununua mbolea bora moja kwa moja toka kwenye
viwanda badala ya kupitia mawakala.
“
Tukiwa na bei nzuri ya zao la chai, tutawavutia vijana wengi kulima na
kuondoa utegemezi wa wazee kuendeleza kuzalisha zao hili muhimu kwa
uchumi wa nchi” alisema Kusaya
Mwisho
Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
Makambako
12.07.2020
No comments :
Post a Comment