Rais
Donald Trump wa Marekani hapo jana alivaa barakoa hadharani kwa mara ya
kwanza ikiwa ni ishara ya kusalimu amri kwa shinikizo la kumtaka kuwa
mfano kwa umma katika wakati janga la virusi vya corona linaendelea
kuitikisa Marekani.
Trump
alionekana akiwa amefunika pua na mdomo kwa kutumia barakoa yenye nembo
ya rais alipotembea hospitali moja ya kijeshi nje kidogo ya mji mkuu
Washington alipokwenda kukutana na maveterani waliojeruhiwa.
Duru
zimearifu kuwa mapema wiki hii wasaidizi wake walimuomba kiongozi huyo
kuvaa barakoa hadharani katika kipindi ambacho visa vya virusi vya
corona vinaongezeka katika baadhi ya majimbo nchini Marekani.
Trump
ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa sharti la kuvaa barakoa, mara kadhaa
ametetea jinsi utawala wake unavyolishughulikia suala la corona licha ya
kwamba Marekani ndiyo taifa linaloongoza duniani kwa maambukizi pamoja
na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19.
Credit:DW
No comments :
Post a Comment