NA. MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
amezindua Mpango wa Uendelezaji wa Viwanda Vidogo na vya Kati wenye
lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji wa ujuzi, masoko na mitaji
katika miradi midogo na vya kati (SMEs) nchini.
Uzinduzi
huo ulifanyika mapema Julai 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kambarage Hazina Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe.
Pia
ulihudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za SIDO, VETA, NEEC, NSSF na
Banki ya AZANIA pamoja na Viongozi na Wawakilishi kutoka taasisi
mbalimbali za Sekta binafsi, Wajasiriamali na Wanafunzi kutoka Vyuo
mbalimbali nchini.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Waziri Mhagama amesema uwepo wa mpango huo utasaidia
kuongeza kasi ya ujenzi na ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira
wezeshi na kuandaa mazingira yenye mfumo wa kibiashara yatakayorahisisha
kutengeneza uzalishaji wenye tija na kuunda soko la bidhaa
utakaoboresha na kuinua maisha ya Watanzania.
“Serikali
imetengeneza fursa za kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli
mbalimbali za maendeleo na kujipatia kipato na kuhakikisha inatatua
changamoto mbalimbali zinazokabili nguvu kazi ya taifa ikiwa ni pamoja
na ukosefu wa elimu na ujuzi wa kutosha pamoja na ukosefu wa mitaji na
masoko ya uhakika wa bidhaa zinazozalishwa”,alisema Waziri Mhagama.
Waziri
alifafanua kuwa mpango umejikita katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali
wanasaidiwa kuongeza ujuzi, kupata uzoefu na kuwawezesha kuhimili
ushindani katika masoko ya ndani na nje. Aidha, Mpango huu pia unalenga
kuwezesha viwanda kupata vifaa vya kisasa kama mitambo kwa ajili ya
kuongeza uzalishaji ili uwe na tija, kutoa mikopo yenye riba nafuu ili
kupanua shughuli za uzalishaji pamoja na kuongeza kinga za hifadhi za
jamii kwa wajasiriamali.
“Kupitia
mpango huu wenye viwanda na wajasiriamali wamepanuliwa fursa ya kupata
mitaji hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wanaohitimu
vyuo katika ngazi mbalimbali,”Alisistiza Waziri
Aliongezea
kuwa, Mfumo unajikita kuwafika wananchi wote bila ubaguzi na matabaka
ya aina yoyote kwa kuzingatia vigezo na masharti nafuu yaliyopo katika
mfumo huu.
“Programu
hii inavunja matabaka baina ya makundi mbalimbali katika jamii na kutoa
fursa sawa kuanzia mtu binafsi hadi vikundi katika kuwapatia mitaji na
ujuzi sawa hivyo tuiunge mkono kwani inawalenga Watanzania wote,”
alisema
Aidha
alibainisha sekta ya viwanda imeendelea kuwa na tija katika kuchangia
ongezeko la Pato la Taifa kwa kuongezeka kwa viwanda vidogo, vya kati na
vikubwa ambapo Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2019
ilikuwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na
ongezeko la asilimia 0.45 na hii ni matokeo ya kuongezeka kwa shughuli
za uzalishaji viwandani katika kipindi hicho pamoja na kasi ya ukuaji wa
thamani ya Uzalishaji Bidhaa Viwandani kwa mwaka 2019 ambayo ilikuwa ni
Shilingi Trilioni 10.2 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 9.6 mwaka
2018, sawa na kasi ya ukuaji wa asilimia 5.8
Waziri
aliendelea kutoa wito kwa taasisi husika kuendelea kutoa elimu kwa
jamii kuhusu fursa zilizopatikana katika program na kuvitumia vyombo vya
habari katika kueleimisha umma kwa malengo ya kuwafikiwa wengi pamoja
na kuzitaka taasisi za kibenki kutoa mikopo kwa wajasiriamali kwa mifumo
rafiki na inayofikika pamoja na kuutaka uongozo wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuwa na program za tathimin utekelezaji wa
mpango kwa vipindi mbalimbali.
Naye
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alieleza furaha
yake ya uwepo wa mpango huo kwani umesadifu mikakakti ya nchi katika
uendelezaji viwanda na kusema imekuja wakati mwafaka kwa kuzingatia
imelenga sekta zenye tija katika kutoa ajira kwa watanzania wengi kwani
imefungamanisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuwa ndizo zenye
mchango mkubwa katika ajira.
“Ni
hakika kuwa, kupitia Mpango huu wa uendelezaji wa viwanda, ajira za
moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika mnyororo mzima wa
thamani wa sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji zitaongezeka na kupunguza
changamoto mbalimbali zinazokabili jamii kutokana na ongezeko la wasio
na ajira nchini,”Alisema waziri Bashungwa.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, Beng’I Issa alisema, mpango umeainisha namna bora ya
kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo la kukuza mitaji na kuimarisha
vyanzo vyao vya mapato na kukuza akiba na mikopo.
No comments :
Post a Comment