Walinzi
nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania
Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam leo.
Walinzi wa nane
wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania Ltd na
wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam leo.
WALINZI
nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania
Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo
shtaka la wizi na utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh bilioni mbili mali
ya NMB benki.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na
Wakili
wa Serikali, Faraja Ngukah imewataja washtakiwa watano ambao ni ndugu
kuwa ni Manjestus Mselema (44), Bernadetha (45) ambaye ni mama wa
nyumbani na Mkazi wa Mbagala, Agnes (29) Hotelia, Oswald Mselema (49)
na Olaph Mselema (35) ambapo wote ni walinzi.
Wengine
ni Beda Mkali (51) ambaye ni CTI Control, Kais Nasibu (35), John
Selestine (45), Edes Hyera (43), Engelbert Masare (45), Bernad Victor
(39) na Sylidion Odil (42), Tulipo Mwamuzi (40) ambaye ni dereva, Grace
Komba (32) Hotelia, Janeth Shilla (59) Wakala wa Kampuni ya Eternal
International Ltd, Godwin (52) Fundi Mwashi na Anold Erio (25), Florah
Mwita (25) mfanyabiashara na Tispo Mwasakieni (27) maarufu Ronic
Kinyozi na mkazi wa Kawe.
Akisoma
hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, wakili
Ngukah amedai, katika tarehe tofauti mwaka 2020, maeneo ya Dar es Salaam
washitakiwa Manjestus, Mwakuzi, Godwin, Anold, Agnes, Mwita, Victor na
Odil walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu ili kufanya kosa la
wizi.
Inadaiwa
kuwa, Juni 8, 2020 huko maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini
Dar es Salaam, washtakiwa waliiba Sh 2,082,000,000 mali ya NMB Benki
Katika
shtaka la tatu imedaiwa Juni 8,2020 huko katika maeneo ya Mbezi Beach
wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa walijipatia Sh
2,082,000,000 mali ya NMB wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa
tangulizi la wizi.
Washtakiwa
hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu mkazi
Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.
Kwa
mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika
na Hakimu Ruboroga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 28, mwaka huu kwa
ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa sababu
mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.
No comments :
Post a Comment