MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia wawili wa China na Mtanzania
mmoja kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 30 gerezani baada ya
kupatikana na hatia ya makosa matano kati ya sita likiwemo la kukwepa
kodi na kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hasara ya Sh.
Bilioni 1.776/=
Aidha
mahakama imeamuru washtakiwa hao wakimaliza kutumikia kifungo walipe
fidia ya kiasi hicho cha fedha walichosababisha hasara.
Washtakiwa
waliohukumiwa leo ambao ni raia wa China ni wafanyabiashara Gu Kai (49)
mkazi wa Kariakoo na Jason Wei (30) anayeishi Tabata Matumbi pamoja na
Jovin James (28) mtanzania anayeishi Tabata.
Aidha mahakama imemuachia huru Leornad Assey (26), baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Hukumu
hiyo imesomwa na hakimu Mkazi Mkuu wa Huruma Shahidi ambaye amesema,
upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake tisa waliofika mahakamani
kutoa ushahidi, wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shtaka kuwa
washtakiwa hao watatu ametenda makosa hayo matano na amewaachia huru
katika kosa moja la kula njama.
Akifafanua
adhabu hiyo Hakimu Shaidi amedai, Katika shtaka la kughushi washtakiwa
watatumikia kifungo cha miaka saba na katika kosa la kutoa nyaraka za
uongo wamehukumiwa miaka saba huku shtaka la kujipatia usajili kwa
udanganyifu miaka miwili kusababisha hasara miaka sana pamoja na kosa la
kukwepa kodi.
Hata hivyo adhabu zote nitaenda pamoja hivyo, watakaa gerezani kwa miaka saba.
Pia, wakati hukumu hiyo inasomwa mshtakiwa Wei hakuwepo mahakamani baada ya kuruka dhamana na mahakama imeamuru atafutwe ili ianze kutumikia kifungo chake.
Aidha
kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Hakimu Shahidi aliuliza kama upande
wa mashtaka walikuwa na lolote la kusema ndipo wakili Anna Chimpaye
akasema hawana kumbukumbu za zamani za washtakiwa lakini wameiomba
mahakama kutoa adhabu kali kwani kosa walilofanya limeitia hasara
serikali.
Katila
kesi ya msingi washtakiwa wote wanadaiwa, mwaka 2014 jijini Dar es
Salaam, walikula njama ya kutenda kosa ambapo wanadaiwa Oktoba 21, 2014
Dar es Salaam walighushi fomu ya taarifa za mteja wakionesha kwamba
kampuni ya Calcare international company ltd imeomba mashine ya EFD kwa
Compulynx Tanzania Ltd wakati siyo kweli.
Katika
shtaka la tatu imedaiwa kuwa siku na mahali hapo mshtakiwa Jovina na
Gu Kai waliwasilisha kwa Compulynx T Ltd fomu ya taarifa ya mteja
wakidai kwamba kampuni ya Calcare iliomba mashine ya EFD huku wakijua
kuwa siyo kweli.
Katika
shtaka la nne imedaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa kwa nia ya
kudanganya walijipatia usajili wa EFD mashine kutoka TRA kwa kujidai
kwamba mashine hiyo ingetumiwa na Calcare huku wakijua kuwa siyo kweli.
Imeendelea
kudaiwa kuwa, kati ya Oktoba 21 2014 na Machi 30 2016 jijini Dar es
Salaam washtakiwa Leornad na Jason wakiwa watu wanaojihusisha na
uendeshaji wa shughuli za kampuni za Tifo Global Mart (Tanzania) na
Lotay Steel ( Tanzania) Ltd kwa nia ya kudaganya walitumia EFD mashine
iliyosajiliwa na Calcare na kukwepa kodi ya sh 1,776,693,465/=
Katika
shtaka la mwisho inadaiwa kuwa, katika kipindi hicho hicho washtakiwa
wote kupitia vitendo vyao waliisababishia TCRA hasara ya Sh.
1,776,693,465/= kwa kusajili EFD mashine na baadae kuitumia kutoa risiti
feki kufuatia mauzo yaliyofanywa na kampuni ya Tifo na Lotay.
Washtakiwa wakipanda kwenye gari la magereza jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuhukumiwa.
No comments :
Post a Comment