Baadhi ya wafanyakazi wa NMB tawi la Mafinga wakibeba sabuni na vitakasa mikono kwa ajili ya shule za msingia Wambi na Manyalala
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB Mafinga wakiwa katika picha ya pamoja
Meneja NMB tawi la Mafinga, Mary Mpasha akizungumza na wanafunzi na walimu juu ya faida ya kuweka fedha kwenye benki ya NMB
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Wambi
Meneja NMB tawi la Mafinga, Mary Mpasha akimkabidhi moja ya sabuni za kunawa mikono Mkurugenzi wa Mji Mafinga, Saada Mwaruka.
…………………………………………………
NA DENIS MLOWE,MUFINDI
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB tawi
la Mafinga wametoa msaada wa sabuni na vitakasa mikono zaidi 100 kwa
shule za msingi za Wambi na Nyamalala zilizoko kwenye halmashauri ya
Mji
Mafinga ili waweze kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya
mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.
Wafanyakazi hao ambao waliombwa
msaada huo na mkurugenzi wa mji wa Mafinga, Saada Mwaruka na kuamua
kuchangishana kama wafanyakazi na kuamua kutoa msaada huo kwa lengo la
kuendelea kuwa karibu zaidi na jamii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Saada Mwaruka,
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mafinga, Mary Mpasha alisema kuwa baada
ya kupata maombi ya kuombwa msaada waliamua kuchangishana na kufanikiwa
kupata vifaa hivyo kwa ajili ya wanafunzi.
Alisema ku wakati wote wafanyakazi
wanaamini katika kugusa na kubadili maisha ya wanajamii, ushiriki wa
Wafanyakazi katika programu za kuisaidia jamii iliwagusa wafanyakazi
hao na kuamua kutoa sehemu ya mishahara yao kwa ajili ya kutoa msaada
kwa shule hizo.
“elimu ni haki ya msingi na
kipengele muhimu cha malengo endelevu ya milenia, tunatambua mchango
muhimu wa shule ya msingi hivyo baada ya serikali kuruhusu masomo
kuendelea umuhimu mkubwa ni kuwafanya wanafunzi wasome katika mazingira
salama Hali iliyotulazimu kuchangishana sehemu ya mishahara na kuwaletea
msaada. huu.” Alisema
Aidha Mpasha aliwataka wanafunzi
hao kuwa mabalozi wazuri wa benki ya NMB na kutoa wito kwao kuwashawishi
wazazi na walezi kuwafungulia akaunti za watoto na masomo kwani
zitawasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye masomo yao.
Akizungumzia msaada huo mkurugenzi
wa Mafinga Mji, Saada Mwaruka aliwapongeza wafanyakazi wa NMB kwa
kuwakumbuka wanafunzi na walimu wa shule hizo kwani utawasaidia kwa
kiasi kikubwa kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona na kuepuka
magonjwa mingine yanayosababishwa na uchafu yakiwemo kuhara.
“Tunaishukuru wafanyakazi wa NMB
Mafinga kwa kwa msaada huu wa sabuni za kunawa na vitakasa mikono kwani
zitatusaidia sana katika kipindi hiki hasa itasaidia pia wanafunzi
kuepuka magonjwa mengine ya kuhara, kipindupindu kusisitiza wanafunzi
kutambua matumizi ya kunawa mikono mara kwa mara,” alisema
Mwaruka alisema kuwa mbali na
kupewa msaadakutoka kwa wafanyakazi lakini Benki ya NMB pia amekuwa
ikiwaunga mkono mara kwa mara na ni msaada mkubwa kwenye jamii ya mkoa
wa Iringa na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana katika
kusaidia makundi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment