Mkurugenzi wa Mafunzo ,utafiti na takwimu ndugu Joshua Matiko akiongea kwenye semina hiyo liyofanyika jijini Dodoma
Washiriki wa semina wakifuatilia kwa makini juu ya mawasilisho toka kwa watoa mada mbalimbali toka OSHA
Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mhandisi Alex Ngata akitoa ufafanuzi juu
ya masuala mbalimbali ya usalama na afya toka kwa washiriki wa semina
waliyotaka kufahamu zaidi
Washiriki
wa semina ya pamoja baina ya OSHA na wawakilishi wa waajiri kutoka
maeneo mbalimbali ya kazi jiji la Dodoma wakisikilza mada zilizokuwa
zinawasilishwa kwenye semina hyo jijini Dodoma.
*************************************
Mwandishi wetu, Dodoma
Mkurugenzi wa Usalama na Afya
Mhandishi Alex Ngata amewataka wadau kuendelea kutoa
ushiriikiano kwa
OSHA ili kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi Maeneo ya kazi, kwa
kuhakikisha kuwa usalama na afya sehemu za kazi zinazingatiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu
Mtendaji Mkuu wa OSHA, kwenye mafunzo ya vision zero mkoani Dodoma
yaliondaliwa na OSHA, Ngata amesema OSHA imeendelea kuboresha huduma
zake kwa wadau hao, hivyo hawanabudi kuhakikisha wanashirikiana naa
OSHA wakati wote kwa kuhakikisha kaguzi zote za kisheria zinafanyika ili
kukidhi matakwa ya sheria. Amesema OSHA imeboresha huduma zake kwa
kuondoa tozo ambazo ni ada ya usajili sehemu za kazi, leseni ya kukidhi
matakwa ya sheria, tozo ya vifaa vya kuzima moto,,fomu ya usajili
amabazo zilikuwa kikwazo kwa waajiri kwa kuziondoa na zingine na hivi
karibuni tumepunguza tozo ya uchunguzi wa ajali sehemu ya kazi ili
kuwezesha waajiri kukidhi matakwa ya sheria.
Naye kwa upande wake
Mkurugenzi wa mafunzo , utafiti na Takwimu Ndugu Joshua Matiko amesema
ili kuweza kufikia malengo hayo,, waajiri nchini wanatakiwa kuweka
mifumo madhubuti ya Kulinda wafanyakazi wakiwa kazini, ikiwemo kuweka
malengo kwenye mipango mikakati yao wanayopanga. Amesema menejiment ndio
wenye jukumu la kusimamia masuala ya usalama sehemu za kazi kwani
wasipoweka juhudi basi nivigumu kufanikiwa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Huduma za tathimin toka mfuko wa fidia (WCF) Dr. Abdulasum Omary amesema
watu takribani milioni 2 .3 wanapoteza maisha sehemu za kazi kila
mwaka kutokana na ajali na magojwa yanayotokana na kazi
Kwa upande wao washiriki wa semina
hiyo wamesema wameshukuru uongozi wa OSHA kwa kuona umuhimu wa
kuendesha semina hiyo kwaajiri aitasaidia kuboresha utendaji wao wa
kazi. Na wamesema semina za mara kwa mara ziawasaidia kupata mambo mengi
ambayo walikuwa hawayafamu.
No comments :
Post a Comment