Friday, July 10, 2020

BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA



**********************************
Balozi wa Ujerumani Nchini, Regine Hess leo tarehe 10 Julai, 2020 amefanya ziara kwenye Banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kupokewa na kutembezwa kwenye mabanda Balozi Hess alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini.

No comments :

Post a Comment