Mwanasheria wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Peace Mpango aweka saini mkataba huo.Wengine
ni baadhi ya viongozi wa Mahakama, wakiwemo watumishi na wageni
waalikwa.
Mwenyekiti wa
Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang CRJE (East Africa)
akisaini mkataba huo. Tukio hili limefanyika kwenye ofisi za Makao
Makuu ya Mahakama ya Tanzania,Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (katikati) jana
alikabidhi mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama kwa
Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang
CRJE(East Africa).Jengo hilo litajengwa kwa muda wa miaka miwili, eneo
la NCC Jijini Dodoma.( Kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,
Mhe. Wilbert Chuma na (kulia) ni Msajili wa Mahakama ya Rufani
Tanzania, Mhe. Kevin Mhina.
Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (katikati) jana Julai
Mosi, mwaka huu, alisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya
Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini
China, Bw.Xie Zhixiang CRJE(East Africa) ambaye hayupo pichani .Jengo
hilo litajengwa kwa muda wa miaka
miwili, eneo la NCC Jijini Dodoma.(
Kushoto) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma na
(kulia) ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Kevin Mhina.
Na Innocent Kansha- Mahakama
Mahakama ya Tanzania jana ilisaini
mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama baina yake na
Kampuni ya Reli kutoka China CRJE (EAST AFRICA) kwa makubaliano ya
kukabidhi kazi hiyo ndani ya miezi 24.
Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za makao makuu ya Mahakama Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusu mkataba
huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Mathias Kabunduguru
alisema anategemea muda waliokubaliana wa kupokea jengo hilo utakuwa kwa
wakati muafaka na litaendanana na hadhi ya Muhimili husika.
‘‘Nategemea kuona tunapokea jengo
zuri lenye ubora halisi unaoendana na thamani ya mkataba huu, kwani
Mahakama ni moja ya nguzo ya Serikali hivyo hatutarajii kuona jengo
lisilo lingana na hadhi ya Muhimili wenyewe,’ alisema Kabunduguru.
Aliongeza kuwa Mahakama ina
wajibu wa kuhakikisha kila mtu anapata haki sio kwa Watanzania tu hata
kwa wageni wanaofika hapa nchini kwa shughuli mbalimbali ikiwemo
uwekezaji na Muhimili huo unatarajia kuwa na jengo hilo liwe chachu ya
uharakishaji wa utoaji haki kama ilivyo katika jukumu lake la msingi
la kikatiba.
Mtendaji huyo aliitaka ofisi ya
Wakala wa Usimamizi wa Majengo Tanzania (TBA) itambue kwamba inayo
wajibu wa kusimamia ujenzi huo sio kwa niaba ya Mahakama ya Tanzania
bali kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani
Mahakama ni sehemu ya kiungo au Muhimili wa Serikali.
‘Mkandarasi unayo kazi kubwa mbele
yako ya kuhakikisha unatekeleza wajibu wako ipasavyo ili uweze kupimwa
kwa thamani ya jengo hili.
‘‘Niwakumbushe tu kwamba leo hii
tumeingia kwenye jukumu kubwa na zito la kutia saini ujenzi huu
tunategemea kuona sio tu kazi iliyo bora bali kazi inayotazamwa na Taifa
zima kwa ujumla, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha ujenzi huu
unafanikiwa kwa kiwango kinachokidhi hadhi ya Mahakama,’’ alisisitiza.
Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli
ya Nchini china CRJE (East Africa) Bw. Xie Zhixiang alihihakikishia
Mahakama kuwa kampuni yao ina uzoefu mkubwa katika kutekeleza miradi
mikubwa ya aina hii, hivyo wanategemea kujenga kwa kiwango cha ubora wa
hali ya juu kulingana na makubalianao ya ujenzi huo.
Kwa upande wa Mkandarasi Mashauri,
Wakala wa Majengo nchini (TBA), ambaye Msanifu wa Majengo Bw. Geofrey
Munyaga alisema tunashukuru kwa kuaminiwa na serikali tupo tayari
kutekeleza jukumu letu kikamilifu kama wasimamizi washauri katika mradi
wa ujenzi huu tutahakikisha tunasimamia ubora wa ujenzi wa jengo hili
unatekelezwa kama ilivyo kusudiwa na Serikali.
Mkataba wa ujenzi huo, umeanza leo na utakamilika ndani ya miaka miwili
No comments :
Post a Comment