**********************************
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
TAASISI ya Mfuko wa
Emerson’s Zanzibar Foundation (EZF) inatarajiwa kutangaza matokeo ya
uhakiki wa filamu 21 zilizowaswilishwa kwenye tunzo ya filamu
iliyokusudiwa kuendeleza na kukuza Vipaji vya Vijana wa Kizanzibari
wanaotengeneza filamu.
Akitoa taarifa yake
kwa vyombo vya habari leo, Mwenyekiti wa Mfuko wa Wakfu wa Emerson’s
Zanzibar Foundation, Said el-Gheithy alisema Wadhamini wa Bodi ya mfuko
huo EZF ulipokea jumla ya filamu 21 kutoka Unguja na Pemba zilizoletwa
katika tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka. Kati ya hizo filamu Nane (8)
pekee ndio zilizokidhi vigezo na sifa zilizowekwa.
“Mwaka huu tunatoa tunzo ya tano….
Filamu
21zilizoandaliwa na Vijana wa Kizanzibari kutoka Unguja na Pemba, nane
pekee ziliweza kupenya kwenye mchujo, na kuhakikiwa na Jopo la Majaji
katika hatua ya mwisho. Matokeo yatatangazwa Julai 4 mwaka huu hapa
Unguja.” Alisema Mwenyekiti wa EZF, Said el-Gheithy.
Aliongeza kuwa:
“Bodi ya Wadhamini ya
Emerson Zanzibar Foundation imekuwa na utaratibu wa kutoa tunzo hiyo
mwezi wa Julai kila mwaka linapofanyika Tamasha la Filamu za Kimataifa
na za Nchi za Majahazi (ZIFF). Lakini mwaka huu Tunzo hiyo itafanyika
kupitia mitandao ya kijamii.
“Tunzo ya Tano kwa mwaka huu itafanyika mitandaoni kutokana na janga la Kirusi cha Covid-19.”, alimalizia Said el-Gheithy.
Kwa upande wake
Meneja Mwandalizi wa shughuli za Tunzo hiyo, Salma Adim alieleza kuwa
tayari majaji wamekamilisha kuzikhakiki filamu hizo. Sasa inasubiriwa
kutangazwa matokeo.
“Filamu
zilizotengenezwa na Chipukizi ndio kauli mbiu ya mwaka huu. Hivyo basi
katika filamu hizo 21 ni nane pekee zilizokidhi vigezo……. .”, alisema
Salma Adim.
Salma Adim aliwataja
Majaji Sita ambao ni wabobezi waliohakiki filamu hizo. Nao ni Helen
Peeks, Bi. Maryam Hamdan, Lisenka Beetsra na Salum Stika ambao
walihakiki hapa Zanzibar. Majaji wengine, Vanessa Victor na Amil Shivji
wao walihakiki filamu hizo kwa njia ya mtandao (online).
Alizitaja filamu hizo zilizoingia Nane Bora ni:
‘Mashaka’, ‘Kipaji’, ‘Urithi wa Mila’, ‘Youth Africa Life’, ‘Kijiji changu’, ‘Fikra yakinifu’, ‘Hofu ya Subira’ na ‘Tubadilike’.
Wadhamini wa bodi
hiyo wameeleza kuwa, Mpewa mstahiki atatunukiwa fedha, Milioni Mbili
(Ml.2), Tunzo maalum ya EZF na cheti cha ushiriki katika tukio adhimu
Mjini Unguja.
Tunzo hiyo imekuwa ikitolewa kila mwaka kuibua vipaji vya Vijana wengi Visiwani Zanzibar.
No comments :
Post a Comment