Mratibu wa Shirika la MAPERECE,
Lavits John Bifandimu, akito mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo
Mabalozi wa Fistula ya Uzazi wilayani Nyamagana.
Mabalozi wa Fistula ya
Uzazi kutoka katika Kata 18 za Wilaya ya Nyamagana wakiwa katika picha
ya pamoja baada ya mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo yalitolewa na
Shirika la MAPERECE la wilayani Magu.
Picha na Baltazar Mashaka
*********************************
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
UELEWA mdogo wa jamii
kuhusu ugonjwa wa fistula ya uzazi visababishi vyake na matibabu yake
unaathiri mtitiriko wa wanawake wengi wenye matatizo hayo kwenda
kutibiwa.
Hayo yalielezwa
jana jijini Mwanza na Daktari Kiongozi wa Wodi ya Magonjwa ya Vizazi na
Uzazi wa Hospitai ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) Dk. Reolvin
Elishaphat, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mabalozi wa Fistula
Wilaya ya Nyamagana.
Mafunzo hayo
yanaendeshwa na Shirika la Kutetea Haki za Wazee, Wanawake na Watoto la
Magu Poverty Focus on Older People Rehabilitation Centre (MAPERECE)
yakilenga kuwaibua wagonjwa wapya wa fistula na kuwapeleka kwenye
matibabu.
Dk. Elishaphath
alisema uelewa wa jamii juu ya ugonjwa wa fistula na wapi matibabu
yake yanapatikana uko chini hali inayosababisha wanawake wanaogua
ugonjwa huo kujenga dhana kuwa wamelogwa, ugonjwa unao waathiri wanawake
wenye kipato kidogo wanaojifungulia kwa waganga wa jadi.
“Ututakuta
wahanga watano, watatu hawajui kusoma wala kuandika, inaonyesha uelewa
wa jamii uko chini kuhusu huduma za afya ya uzazi.Hivyo mafunzo haya
tunataka watu waelewe tatizo la fistula,chanzo chake, dalili, madhara na
matibabu yake, dalili, madhara ili kuondoa dhana ya kulogwa ama
unasababishwa kujamiiana na wanaume wengi,”alisema.
Kiongozi huyo
wa wodi ya magonjwa ya vizazi na uzazi alisema ugonjwa wa fistula
unatibika ambapo mafunzo yanayotolewa kwa mabalozi wa fistula
yatawasaidia kutoa rufaa na usafiri kwa wagonjwa kwenda kwenye
hospitali zinazotoa huduma ya tiba ya fistula.
Kwa mujibu wa
takwimu za Wizara ya Afya, mwaka 2015 wanawake 1,337 walijitokeza
kutibiwa fistula , 2016 waliopata tiba ni 1,356 ambapo 2017 idadi
ilishuka na wanawake 1,060, mwaka walitibiwa 900 na mwaka jana
waliopata tiba walikuwa 852.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa MAPERECE, Julius Mwongela alisema tatizo la ugonjwa wa
fistula ya uzazi ni kubwa kwenye jamii hasa vijijini kutokana na
changamoto mbalimbali za ukosefu wa elimu, uchumi na huduma duni za afya
ya uzazi zinazotolewa.
Alisema wahanga
wakubwa na walio kwenye hatari ya kupata fistula ni wasichana wa umri
chini ya miaka 18 kutokana na kupata mimba za utotoni ambapo nyonga zao
zinakuwa hazijakomaa na hivyo kupata majeraha makubwa kulinganisha na
wenye umri wa zazidi ya miaka 18.
“Hapa tunapiga
debe kuishawishi serikali kulibeba suala la fistula liingizwe kwenye
Afya ya Mama na Mtoto kwa sababu wanawake wenye tatizo hilo wametengwa
wakati yote yanahusu uzazi.Wizara ikilichukua watatambuliwa na kutibiwa
bure vinginevyo itakuwa ni kuwabeza wanawake wenye fistula,”alisema
Mwongela.
Aidha alidai
kuwa changamoto ya kuwabaini wagonjwa wa fistula ni kikwazo kwani wengi
wanaopata tatizo hilo hufanya siri ama wanakuwa wmeathirika kiakili na
kisaikolojia na hivyo kutojiweka wazi.
Akifungua
mafunzo hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk. Juma
Mfanga, Mratibu wa Afya ya Uzazi Wilaya ya Nyamagana, Bertha Yohana
aliwataka mabalozi hao wa fistula elimu hiyo waitumie kuleta mabadiliko
chanya kwenye na kuibua wagonjwa wapya
No comments :
Post a Comment