Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abbasi,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati
akitangaza siri 10 za Tanzania kung’ara na kuingia Uchumi wa kati miaka
mitano kabla ya kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abbasi,akifafanua jambo zaidi kwa waandishi wa habari jijini Dodoma
wakati akitangaza siri 10 za Tanzania kung’ara na kuingia Uchumi wa kati
miaka mitano kabla ya kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya
2025.
………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Tanzania yavunja
rekodi kwa kuingia kwenye uchumi wa kati miaka mitano kabla ya lengo la
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 jambo ambalo linaifanya Tanzania
kuandika historia dunia.
Kauli hiyo
inatokana na Benki ya Dunia kuitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 50
duniani za uchumi wa kipato cha kati, ikiwa ni ya pili baada ya Kenya
katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, baada ya ukuaji wa uchumi
unaosukuma pato la mwananchi kukua (Per capita GNI) mwaka 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abbasi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, amesema kuwa
kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 katika ukurasa wa pili,
kipengele 1.2 Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na kuwa na nchi
ambayo umaskini unapungua, uchumi imara unaojengwa na kuimarika kwa
uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo.
Dkt. Abbasi
ameeleza kuwa uchumi wa kipato cha kati umegawanyika katika madaraja
mawili daraja la chini ambapo ni kuanzia dola za Kimarekani 1036 hadi
4045 na daraja la juu ni dola 4046 hadi 12,535 na mwaka huu Tanzania
imepanda daraja kuwa uchumi wa kipato cha kati daraja la chini, pamoja
na nchi za Algeria na Benin.
Pia Dkt. Abbasi
amebainisha siri 10 zilizoisaidia Tanzania kutajwa kufikia daraja la
uchumi wa kipato cha kati na Benki ya Dunia hapo Julai 1, 2020 kuwa ni
nchi yenye amani na utulivu, na hivyo ni msingi muhimu nyuma ya
mafanikio ya nchi ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kipato cha kati
kwani bila amani hakuna kufanyakazi, hakuna kuzalisha na hakuna
kuongeza kipato.
“hivyo viongozi,
wanahabari na wananchi kwa ujumla niwasisitizwa kuwekeza akili zao
katika kuimarisha amani iliyopo na kukataa chokochoko zozote zile
zinazoweza kuharibu misingi ya maendeleo”ametoa wito Dkt. Abbas.
Aidha Dkt. Abbasi
amesema siri nyingine ni utekelezaji usioyumba, katika miaka 59 ya
Uhuru na mitano ya Awamu ya Tano Serikali imejitahidi kusimamia eneo
hilo kwa kuhakikisha mipango inayowekwa inatekelezwa kwa kina (3feet implementation).
Dkt. Abbasi
amesema kuwa azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi, kutekeleza
miiko ya uongozi, kuwekeza kwenye miradi inayochemsha uchumi, maendeleo
ya vitu na sekta binafsi yenye tija ndio chachu ya Tanzania kufikia hapa
ilipo leo.
No comments :
Post a Comment