Sunday, July 5, 2020

TUMEJIPANGA KUWAHUDUMIA WANANCHI SABASABA- NHIF





 Picha mbalimbali za wananchi wakipata huduma katika Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Maonesho ya Biashara Kimataifa Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), unawahimiza wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na washiriki wote wa Maonesho ya Sabasaba kutumia fursa hiyo ili kupata elimu na kujisajili na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Akizungumzia ushiriki wa NHIF katika maonesho hayo, Meneja Uhusiano wa Mfuko Bi. Anjela Mziray, amesema kuwa azma kubwa ya Mfuko ni kuhakikisha unasogeza huduma kwa wananchi na kurahisisha mchakato wa usajili ili kila mwananchi afanikishe kujiunga na huduma zake.

“Maonyesho haya kwetu sisi NHIF ni fursa kubwa ya kusogeza na kuwafikia wananchi wengi ambao wakati mwingine imekuwa ngumu kutufikia na katika kipindi hiki tunazo huduma mbalimbali zinazompa kila mwananchi nafasi ya kujiunga tofauti na hapo zamani,’ alisema Bi. Mziray.

Alisema kuwa makundi yanayosajiliwa katika banda la NHIF ndani ya viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ni pamoja na mwananchi mmoja mmoja kupitia vifurushi vya Wekeza, Najali na Timiza ambavyo vinatoa fursa kwa kila mwananchi kujiunga kulingana na mahitaji yake.

Makundi mengine ni watoto chini ya umri wa miaka 18, makundi ya Machinga, Bodaboda, Madereva, Makampuni Binafsi na makundi mengine.

“Natumia fursa hii kuwakaribisha wananchi wote katika banda letu ambalo lipo nyuma ya banda la Jakaya Kikwete, ili kupata uelewa wa huduma za Mfuko lakini pia kujisajili,  alisema Bi. Mziray.

No comments :

Post a Comment