Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa Kassim akifurahi jambo wakati akisikiliza maelezo
kutoka kwa Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB -
Alfred Shao (kulia), alipotembelea Banda la NMB kwenye maonesho ya Saba
Saba. Katikati ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB -
Benedicto Baragomwa.
====== ======= ======== ========
Maendeleo
makubwa yaliyopatikana nchini katika kipindi cha kwanza cha uongozi wa
Serikali ya Awamu ya Tano, yamechangiwa kwa namna mbalimbali na kwa
kiasi kikubwa na mchango wa Benki ya NMB. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema hayo, alipotembelea banda la Benki ya NMB inayoshiriki Maonyesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yaliyoanza wiki
iliyopita na yanaendelea hadi tarehe 13/07/2020.
.
Hii ni pamoja na uzalendo wa viongozi wake chini ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo - Bi.
Ruth Zaipuna, ambaye Waziri Mkuu alisema ni kati ya Wakurugenzi wanne
Watanzania waliyoisaidia Serikali kuwahudumia vizuri na kuwaletea
maendeleo Watanzania.
“NMB
ni benki yetu…na Mkurugenzi wake ni mmoja wa Wakurugenzi sita
walioichangia sana serikali ambapo wanne ni Watanzania…Kamwambieni
Mkurugenzi wenu, nampongeza sana kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya,
serikali inaitambua na kwakweli anafanya kazi nzuri sana,” Waziri Mkuu Majaliwa aliwaambia wafanyakazi wa benki waliokuwa kwenye banda la benki hiyo katika viwanja vya Saba Saba
Pongezi
hizo alizitoa baada ya kumsikiliza Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na
Serikali wa NMB - Bw. Alfred Shao, katika hotuba yake fupi ya
kumkaribisha kiongozi huyo na kumpa maelezo mafupi ya mchango wa benki
hiyo katika ujenzi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Benki
hiyo ni moja ya taasisi kubwa za fedha nchini ambayo tangu kubinafishwa
kwake, imelihudumia taifa kikamilifu na kuchangia kwa kiasi kikubwa
ukuaji wa uchumi wa nch. Maendeleo ya wananchi wa kawaida pamoja na
sekta mbalimbali kama vile kilimo, kupitia huduma zake nyingi na zenye
tija hasa zile za mikopo.
Kwa
mujibu wa Bw. Shao, mambo yaliyofanywa na Benki ya NMB kupitia uwekezaji
kwenye maeneo mengi ya kimaendeleo kwa miaka minne mpaka sasa hivi ni
mengi, ikiwemo mikopo kwa sekta binafsi yenye thamani ya TZS 2 trilioni
ambayo pia imesaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia ujenzi wa uchumi wa
viwanda. Benki hiyo ambayo kwa zaidi ya miaka kumi imekuwa kiongoza kwa
kutengeneza faida kubwa, imetoa TZS 800 bilioni kusaidia kilimo na
mnyororo wa thamani katika sekta hiyo.
Bw.
Shao alisema mazao yaliyonufaika sana na mchango huo wa fedha kutoka NMB
ni pamoja na pamba, mihogo, alizeti, kahawa na korosho.
“Benki
ya NMB imeisaidia pia serikali kupitia kuchangia utekelezaji wa miradi
mikubwa ya kimkakati. Zaidi ya TZS 1.2 trilioni imeishatolewa kusaidia
miradi mikubwa ya serikali kama umeme, miradi ya maji, reli ya umeme
almaarufu SGR,” kiongozi huyo mwandamizi alisema.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia alitoa pongezi maalumu kwa NMB kutokana na jinsi
benki hiyo inavyopambana kuboresha maisha ya Watanzania hasa wale wa
vipato vya chini wanaoishi vijijini. “Pia nawapongeza mlivyosaidia
wananchi wa vijijini kufungua akaunti kupitia AMCOS,” alisema.
No comments :
Post a Comment