Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akiongea na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati
walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini, Mhe. Wang
Ke akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati
Walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
……………………………………………………………………….
Tanzania na China zimeahidi
kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa
nchi hizo
zinakuwa na maendeleo endelevu.
Makubaliano hayo yamefanywa na
Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati alipokutana kwa mazungumzo
na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge leo jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge
amesema kuwa wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la namna ya
kutekeleza nia ya Viongozi Wakuu wa nchii za China na Tanzania (Rais wa
China, Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. John Joseph Pombe Maufuli) ya kupunguza madhara yatokanayo na
ugonjwa wa COVID 19 ikiwemo kufutiwa na kusamehewa madeni.
Naishukuru Serikali ya China kwa
uhusiano na ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa Tanzania. Uhusiano
huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa
ukiimarika siku hadi siku na kuahidi kuwa serikali ya Tanzania itaendela
kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia kati yake na China.
Pamoja na mambo mengine,
mazungumzo yalijadili masuala ya biashara na uwekezaji, mradi wa nyumba
25 za wataalum wa Afya zilizopo Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Balozi Wang Ke
pamoja na mambo mengine, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada
ilizochukua katika kukukuza uchumi wake hadi kufikia uchumi wa kati,
pamoja na mapambano dhidi ya COVID 19.
“Leo nimekutana na Katibu Mkuu wa
Mambo ya Nje, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge na kuongea mambo mbalimbali
ya ushirikiano na tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada
ilizochukua katika kufanya kazi kwa bidii na kukuza uchumi wake hadi
kufikia uchumi wa kati, pamoja na hatua ilizochukua katika kupambana na
janga la COVID 19 ambapo tumefurahishwa kuona janga la COVID 19
limeisha,” Amesema Balozi Ke.
Balozi Ke ameongeza kuwa
wamekubaliana katika maongezi hayo pia kuendeleza ushirikiano wa kufanya
kazi kwa pamoja kwa manufaa ya mataifa mawili (Tanzania na China) ili
kuhakikisha uhusiano na ushirikiano unazidi kukua na kuimarika.
Tanzania na China zimekuwa
zikishirikiana katika sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, miradi ya
mikopo nafuu na misaada, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
Uchukuzi, Afya, Utalii na utamaduni.
China na Tanzania zilianzisha mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964.
No comments :
Post a Comment