Kaimu
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Benedicto Baragomwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Ummy Mwalimu wakiwa
wameshika madawati yaliyokabidhiwa na benki ya NMB kwa ajili ya shule
saba za jijini Tanga kwenye hafla ya makabidhiano yaliyofanyika katika
shule sekondari Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga. Kutoka kushoto ni
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro, Katikati mwenye miwani
ni Meneja wa NMB Madaraka – Elizabeth Chawinga na Mwisho kulia ni
Mkurugenzi wa jiji la Tanga – David Mayeji.
Benki
ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya shilingi Milioni 36 kwa shule
Saba za sekondari; Kirare, Japan, Chongoleani, Nguvumali, Pongwe na
Galanos za Jijini Tanga, kwa kuzipatia madawati 250 pamoja na mabati 352
ili kutatua changamoto za kielimu.
Akikabidhi
msaada huo katika shule ya sekondari ya Pongwe kwa Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto - Ummy Mwalimu, Kaimu Afisa
Mkuu wa fedha wa benki hiyo - Benedicto Baragomwa alisema, wamekuwa
mstari wa mbele kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kwa
wananchi.
Alisema
kwa upande wa sekta ya elimu, kipaumbele wamekiweka kwenye madawati,
vifaa vya kuezekea huku kwenye afya wakitoa vifaa vya tiba kama vitanda
vya kujifungulia wakina mama na vitanda vya wagonjwa na magodoro yake
vilevile na kusaidia majanga yanayoipata nchi.
Aidha
aliongeza kuwa, katika kipindi cha miaka minne benki hiyo imekwisha
changia zaidi ya shilingi Bilioni nne kusaidia jamii katika ununuzi wa
vifaa tiba 330 kwa hospitali na vituo vya Afya, zaidi ya madawati 31,150
pamoja na kompyuta1,150 nchi nzima.
"Kwa
mwaka huu NMB imetenga zaidi ya shilingi Bilioni moja kwa ajili ya
kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu" alisema Baragomwa.
Kwa
upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto -
Ummy Mwalimu alisema kuwa elimu bure imeweza kusaidia watoto wengi wa
kike kupata fursa ya elimu tofauti na hapo awali.
No comments :
Post a Comment