Friday, July 10, 2020

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI BALOZI WA UMOJA WA ULAYA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI MANFREDO FANTI ALIPOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


Kamishna Msaidizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dionisia Mjema, akimuongoza Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti, kutembelea na kupata maelezo mbalimbali ya huduma na elimu inayotolewa na wizara hiyo pamoja na Taasisi zake wakati balozi huyo alipotembelea Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Bw. David Magabe, akitoa ufafanuzi kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe.  Manfredo Fanti, kuhusu namna Serikali, Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi zinavyoweza kupata mitaji ya kugharamia miradi ya maendeleo kupitia masoko ya mitaji, wakati balozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango , Bw. Benny Mwaipaja, akimkabidhi Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti machapisho mbalimbali ya wizara hiyo wakati balozi huyo alipotembelea banda la wizara katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, (wa pili kushoto) akiwaongoza wawakilishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kumkaribisha Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti, alipofika kujionea huduma na elimu inayotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bi. Josephine Majura.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments :

Post a Comment