Sunday, July 12, 2020

TANTRADE YAISHUKURU NBC KWA KUWADHAMINI WAJASIRIAMALI MAONESHO YA BIASHARA 2020


Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara ya Masono Tanzania (TanTrade)  Bi Latifa Khamis, (watatu kushoto), akipokea risiti ya malipo ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Meneja Uhusiano, William Kalaghe (kushoto) wakati viongozi wa mamlaka hiyo walipotembelea banda la NBC. Wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja bidhaa wa benki hiyo, Jonathan Bitababaje, Kaimu Meneja Uendelezaji Biashara Bi Masha Hussein na Meneja Matawi wa NBC, Godhard Hunja.

Mamlaka ya Uendelezaji Biashara na Masoko Tanzania (TanTrade) imeishukuru benki ya
NBC
kwa kuwawezesha wajasiriamali kushiriki maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa
ya Dar es Salaam mwaka huu wa 2020.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa TanTrade  Bi Latifa Khamis wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye viwanja vya Julius Nyerere, maarufu sabasaba ili kutoa shukran kufuatia udhamini huo.
“NBC ni miongoni mwa taasisi ambazo zimekuwa zikituunga mkono kwa takriban miaka minne mfululizo, ni wadau wakubwa wa maonesho haya ya sabasaba, kupitia udhamini wao wa shilingi milioni 80 wamewawezesha wajasiriamali kushiriki maonesho haya
wakiwa na bidhaa zenye viwango vinavyohitajika bidhaa zao ziko kwenye standards za kimataifa.” Alisema.
Kwa upande wake, Bw. William Kalaghe aliwapongeza Tantrade kwa kuwezesha maonesho kufanyika katika kipindi kifupi na ndio maana NBC iliamua kuwa sehemu ya
taasisi zilizounga mkono maonesho haya.
“Sisi
ni wadau katika maonesho haya, hatuko hapa tu ili tuonekane bali ni moja ya wachezaji
muhimu katika kukuzxa uchumi wan chi hivyo tuko hapa kuwaenzi na kuwatunza
wajasiriamali ili waweze kutekeleza shughuli zao na tunatoa wito kwao waendelee
kushirikiana na TanTrade.”

No comments :

Post a Comment