Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari
Mgumba,akizungumza na wadau wa Tasnia ya mkonge katika mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkonge Bi
Mariamu Mkumbi wakati akihutubia wadau wa Tasnia ya mkonge katika
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Royal Village Jijini
Dodoma
Wakuu wa Mikoa mbalimbali
wakisikiliza mawasilisho mbalimbali katika mkutano wa wadau wa tasnia ya
mkonge uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari
Mgumba (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya
wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano wa wadau wa tasnia ya mkonge
uliofanyika leo Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna, Dodoma
Serikali yakutana
na wadau wa Mkonge nchini ili kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto
zinazoikabili tasnia ya hiyo ili kuongeza tija katika uzalishaji,
ajira na kukuza sekta ya
viwanda, pato la mkulima na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo
imebainishwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary
wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa mkonge nchini.
Aidha Mhe. Mgumba
amesema kuwa serikali imeanda mikakati katika zao la mkonge ili
kuongeza tija na uzalishaji kwa kuanzisha vitalu vya mbegu ya mkonge
katika Halmashauri zote amabako zao la mkonge linastawi.
Mhe. Mgumba
amesema kuwa kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Mlingano
uzalishaji wa mbegu bora umeanza ili ziweze kuzalishwa kwa wingi.
Mhe. Mguma
ameeleza kuwa serikali inafanya uhakiki wa mashamba ya Mkonge
yaliyobinafsishwa ili yaweze kuzalisha mkonge kama ilivyokubaliwa kwenye
mikataba.
Pia amesema kuwa
selikari imejipanga Kutoa elimu kwa maafisa ugani katika vijiji na kata
kwenye maeeo yanayolima mkonge ili kuwajengea uwezo wa kuwahudumia
wanachi katika kulima zao la mkonge.
“serikali
itaongeza Bajeti nakuwezesha Kituo cha Utafiti Mlingano kufanya utafiti
wa aina mbalimbali za mbegu ya mkonge na kuzisambaza kwa wakulima bila
kusahau Kulinda ardhi ya kilimo ili isibadilishwe matumizi ambapo
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeshaanza kufanya maboresho katika
Sera na Sheria zake”, ameweka wazi Mhe. Mgumba.
Mhe. Mgumba
ameongeza kuwa watahakikisha wanahimiza na kushawishi wawekezaji
kuwekeza mnyororo wa thamani wa Tasnia ya Mkonge hususan kwenye viwanda
na teknolojia bora za uzalishaji wa bidhaa za mkonge ikiwemo magunia,
mazuria, matofali, mapambo, n.k ili kupanua soko la ndani na nje.
Hata hivyo Mhe.
Mgumba amesema kuwa watanzania kwa kushirikiana na serikali wanatakiwa
kulinda viwanda vya ndani kwa kuongeza tozo na kodi kwa bidhaa mbadala
wa mkonge zinazoingizwa hapa nchini kutoka nje ya nchi.
Naye Mwenyekiti
wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Evarist
Ndikilo ametoa wito kwa wadau wa mkonge kuwa wawazi katika mkutano huo
ili baada ya kikao hicho basi wakatekeleze yale yatakayo kuwa
yameamuliwa katika mkutano huo ili kufufua kilimo cha mkonge nchini na
shabaha kubwa ikiwa ni kurudisha taswira ya zao hilo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkonge Tanzania, Bi. Mariam Mkumbi
amesema kuwa kutokana na zao la mkonge kuwa moja kati ya mazao saba ya
kimkakati hapa nchini Pamoja na maelekezo ya serikali ya kuongeza
uzalishaji wa zao la mkonge kutoka tani 36,000 mwaka 2019 na kufikia
tani 120,000 mwaka 2025.
“Bodi ya Mkonge
Tanzania imeandaamkakati wa kurudisha hadhi ya zao la mkonge kama ilivyo
kuwa katika miaka ya 1960 ambapo Tanzania ilikuwa inaongoza kwa
uzalishaji na ubora wa mkonge duniani”, ameeleza Bi. Mkumbi.
Bi. Mkumbi
ameongeza kuwa uzalishaji huo unalenga kuhusisha takribani tani 62,331
kutoka kwa wazalishaji waliopo katika mashamba makubwa na tani 60,256.9
na zaidi ya hapo kutoka kwa wakulima wadogo katika mikoa 16 ndani ya
kanda sita zilizoainishwa katika mpango huo wa ndani ya Tanzania Bara
ambao watahamasishwa kpitia mpango huo.
Itakumbukwa kuwa
zao la mkonge lina historia ndefu nchini kwani mwaka 1964 Tanzania
iliweza kuzalisha jumla ya Tani 230,000 na kuongoza Duniani kwa
uzalishaji wa zao la mkonge. Kipindi hicho mkonge ulikuwa unachangia
asilimia 65% ya fedha za kigeni nchini.
No comments :
Post a Comment