Mkurugenzi wa Kampuni ya Geared Consulting Engineers ltd warda
Meshamerk akizungumzia namna serikali ya awamu ya tano ilivyotoa fursa
kwa wahandisi wa ndani kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.
************************************
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Kampuni ya Ushauri
wa masuala ya umeme ya (GEARED Consulting Engineers LTD) Mhandisi warda
Ester Meshamerk ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fursa
kwa wahandisi wa ndani nakuamini kutekeleza miradi mikubwa ya
kimkakati.
Amesema katika kipindi hiki cha
serikali ya awamu ya tano serikali imetambua uwezo mkubwa walionao
wahandisi wa ndani nakutoa fursa ya kuwapa miradi mbalimbali mikubwa
kuitekeleza hapa nchini.
Mkurugenzi Ambaye ni Mhandisi na
mtaalamu mshauri wa masuala ya umeme warda aliyasema hayo Jijini Dar es
Salaam mbele ya waandishi wa haabri .ambapo alisema anaipongeza Sana
serikali kwa kuwaamini huku akitolea mfano kampuni yake kupewa mradi
mkuwa wa Hospitali ya Kwanga iliyopo Msoma mkoani Mara.
“Wazawa tunapewa fursa tena kubwa
katika kipindi hiki hakuna longolongo kwani ukikidhi vigenzo vyao tu
unapata kazi bila shaka yeyote .mfano mimi licha ya miradi mingine mingi
lakini serikali imeniamini na hivi Sasa kupitia kampuni yangu
tunasimamia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Kwanga unaoendelea
katika eneo la umeme.”alisema Mhandisi warda
Nakuongeza kuwa “Najitahidi
kuukimbiza mradi ule ili uweze kukamilika mapema ili wananchi wa mkoa wa
Mara na viunga vyake waweze kupata huduma pale.amesema
Pia alisema licha ya kusimamia
miradi mbalimbali hapa nchini lakini pia kampuni yake kutokana na kazi
nzuri inazofanya imeweza kuaminika na kupata kazi katika nchi jirani
Kama vile Malawi,Zambia na kungineko na hata Visiwani Zanzibar.
Wakati huohuo Mhandisi warda
alisema kwakuwa kampuni yake moja ya kazi zake ni kusanifu Miundombinu
ya umeme, na katika kuhakikisha vijana wanasoma masuala ya Ushauri
hususani kwenye eneo la umeme wanaiva vizuri ameandaa semina ya kuwapiga
msasa vijana hao ambao wako vyuoni.
Alisema semina hiyo itafanyika
Julau 16 katika ukumbi uliopo DIT kwa maana Dar es Salaam Information
Teknoloji ambapo vijana kutoka vyuo mbalimbali watakutanishwa hapo ili
kuweza kupata madini mbalimbali katika sekta ya umeme .
“Semina hii italenga kuwapa
ujuzi,na hasa wa kujua mabadiliko ya nyaya za umeme .miundombinu mingine
kuhusu umeme hivyo semina hii itafanyika julai 16 pale DIT na lengo
kubwa nikubadilishana uzoefu.na hasa kujua sokoni kunanini na chuoni
kunanini.”amesema Mhandisi warda
mkurugenzi alimaliza kwa kuwataka
vijana hao wakitanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani watakuja kupata
elimu ya kutosha hususani katika eneo la umeme.
No comments :
Post a Comment