Sunday, July 12, 2020

RAIS MAGUFULI AAGIZA COSOTA KUHAMIA WIZARA YA HABARI KUTOKA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA



……………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Chamwino Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa kuihamisha COSOTA inayoshughulikia masuala ya wasanii kwa kumwagiza Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi kuanza utaratibu wa kuhamishwa kwa shughuli zote za COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na kuhamia Wizara ya
Habari na kumtaka Waziri Mwakyembe kulishughulikia suala hilo.
Agizo hilo limetolewa leo wakati wa Wajumbe 6500 walipotembelea Ikulu ya Chamwino na kuweka udongo kama ishara ya kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma
Aidh Rais Magufuli ameagiza Kabla ya jumapili ijayo COSOTA iwe imeshahamia kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ili wasanii kuweza kupata faida ya kazi zao wanazofanya.
Rais Magufuli amesema amefurahishwa kuwaona wasanii ambao wamekuwa na tofauti zao(‘bifu) kwa muda mrefu wakikaa pamoja kwa amani na kufurahiana, Wasanii hao ni Ali Kiba, Diamond Platnumz na Harmonizer.
Lakini pia Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali inataka kuamia Dodoma
zipo nchi mbalimbali zilijipanga kuja kujengea Ikulu akasema hii ni dharau, ukiruhusu jirani akutandikie Kitanda unacholala na mkeo atafanya maajabu, akishindwa kuchukua mke wako atachukua mabinti zako.
“Tumeamua Ikulu hii ijengwe na watanzania wenyewe, haina maana jirani akutandikie mpaka kitanda, siku nyingine atafanya maajabu, Tumeamua tujenge wenyewe, Watanzania tunaweza kila kitu Ndani ya miezi sita itakuwa imekamilika “, amesemaRais Magufuli.
“Katika miaka yangu yote nikiwa Waziri sijawahi kugombea nafasi ya NEC kwahiyo sijawahi kuwa mjumbe wa NEC wala Kamati Kuu, waliponiomba nigombee nilikataa, maana kama nimeshindwa kumshauri Rais kwenye Baraza la Mawaziri ndio nitaweza kumshauri nikiwa NEC?” -ameeleza Rais Magufuli
“Nimewakaribisha hapa kwa kazi moja tu hii ni Ikulu yenu, mimi ni mpangaji tu na ndiyo maana sikubagua hata wa vyama vingine nimewakaribisha kwa kutambua tuna wajibu wa kujenga Tanzania moja” amesema Rais Magufuli
Naye Mgombea mwenza CCM ambaye pia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa alipteuliwa aliyemteua hakujua utendaji kazi wake lakini nguvu yake ya utendaji kazi imetoka kwa wanawake .
“ Hivyo asante kwa kuniteua tena kwa mara ya pili ninakuahidi kuwa nitakuwa bega kwa bega na wewe na kufanya kazi bila kuchoka ili kuinufaisha Tanzania yetu,” Mhe. Samia
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amempongeza Rais Magufuli na watanzania wote kutokana na ile taarifa ya Benki ya Dunia ya kwamba Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati si jambo dogo japo anaona katika mitandao wanabeza na yeye akasema anadhani ni wagonjwa wa akili.
Huku Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa ametoa witokwa kw wajumbe wote wa CCM kuondoa tofauti zao na kuwa wamoja ili kuimarisha mshikamano utakao leta kuwashinda wapinzani katika majimbo yote.
Kwa Upande wake Mgombea Urais CCM Zanzanibar Dkt. Hussen Mwinyi ametoa rai kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, kuwa pamoja na wao katika uchaguzi mku kule Zanzibar ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo amemshauri Rais John Magufuli, kufikiria uwepo wa kongamano la vyama vya siasa nchini ambalo litawajumuisha vyama vyote vya upinzani na kujadili masuala muhimu ya Kitaifa.
Cheyo amemuomba Rais Magufuli kuwezesha kuwepo kwa uwakilishi wa wabunge wakulima watakaopaza sauti kwa ajili ya wakulima wa mazao mbalimbali yanayoulimwa nchini ili yaweze kuuzwa kwa bei nzuri na mkulima afaidike.
Mhe. Cheyo amerudia kauli yake kuwa UDP inaiunga mkono CCM katika Uchaguzi wa mwaka huu hususan katika nafasi ya Urais.

No comments :

Post a Comment