***********************************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameipongeza Benki Kuu ya
Tanzania, mabenki na sekta ya fedha kwa ujumla kwa
mchango wao katika
kuiwezesha Tanzania kuingia katika kundi la nchi za uchumi wa kati.
Dkt. Magufuli ametoa pongezi hizo
katika mazungumzo yake na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens
Luoga, tarehe 2 Julai 2020..
Dkt. Magufuli amemtaka Gavana
Luoga kumfikishia salamu zake za pongezi kwa wafanyakazi wa Benki Kuu na
kwa sekta ya fedha kwa ujumla.
Aidha, amezitaka Benki Kuu, mabenki na sekta ya fedha kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi kwa maendeleo ya taifa letu.
Mnamo Julai 1, 2020, Benki ya
Dunia ilitangaza kwamba Tanzania imeingia katika kundi la nchi za uchumi
wa kati. Benki ya Dunia inaitambua nchi kwamba imeingia katika kundi la
chini la nchi za uchumi wa kati kama wastani wa pato la mtu kwa mwaka
ni kati ya dola za Kimarekani 1,036 na dola 4,045.
No comments :
Post a Comment