Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonyesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam , Barabara ya Kilwa
jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kuranda na kuweka urembo
kwenye mbao wakati alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya
Viwanda Vidogovidogo (SIDO) kabla ya kufungua Maonyesho ya 44 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam , Barabara ya Kilwa jijini Dar
es salaam, Julai 3, 2020. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,
Innocent Bashungwa na wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Shoma Kibende. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipunga baada ya kukata utepe wakati
alipofungua Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ,
Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020. Wengine pichani
kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhandisi Stella
Manyanya, Waziri wa Biashara na Viwanda, Innocent Bashungwa,Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro na kulia ni
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua Maonyesho ya 44 ya
Biashara ya Kimataifa ya Nnee ya Dar es salaam , Barabara ya Kilwa
jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020.Wengine pichani kutoka kushoto ni
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhandisi Stella Manyanay, Waziri wa
Biashara na Viwanda, Innocent BashungwaNaibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro na kuliani Naibu Waziri wa Nishati,
Subira Mgalu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
***********************************
*Asema Serikali itaendelea kuviwezesha viwanda vidogo, vya kati
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na
wezeshi ili kuviwezesha viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati kukua na
kufanya kazi kwa tija zaidi.
Ametoa kauli
hiyo leo jioni (Ijumaa, Julai 3, 2020) wakati akifungua rasmi Maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (44TH DITF) yaliyoanza
Julai mosi, 2020 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu
ambaye amefungua maonesho hayo kwa niaba ya Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli amesema ili nchi iweze kuwa na mafanikio makubwa, taasisi za
kifedha hazina budi kuweka mikakati ya kutoa huduma ya mikopo rafiki ili
kuwezesha ukuaji wa viwanda kwa kuzingatia viwanda vidogo na vya kati
ikiwemo vinavyoratibiwa na SIDO katika kila mkoa.
“Taswira hii
ya maendeleo ya sekta ya viwanda inafanana na taswira ya maendeleo ya
viwanda katika nchi karibu zote duniani. Kwa mfano, Japan, viwanda
vidogo sana, vidogo na vya kati vinachukua takribani asilimia 99 ya
sekta ya viwanda; Kenya asilimia 98; Malaysia asilimia 97.3; Indonesia
asilimia 99.9; Canada asilimia 98 na Ujerumani asilimia 99.”
Amesema
Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya biashara na viwanda nchini ili
kuchochea maendeleo ya nchi kwa ujumla. Akielezea mafanikio ya Serikali
katika kipindi cha miaka mitano, Waziri Mkuu amesema: “Jumla ya viwanda
vipya 8,477 vimejengwa na kuchangia kuzalisha ajira mpya 482,601…
mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2019 ulikua
kwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na
ongezeko la asilimia 0.45.”
Amesema
mchango huo, ni matokeo ya kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji wa
bidhaa viwandani nchini ambao unaendelea kuimarika na kukua vizuri.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu amesema mwaka 2019, bidhaa za viwanda zilikuwa
na thamani ya sh. trilioni 10.2 ikilinganishwa na sh. trilioni 9.6
mwaka 2018 ambao ukuaji wake ni sawa na asilimia 5.8.
Kuhusu
viwanda vidogo na biashara ndogo, Waziri Mkuu amesema sekta hiyo
inaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa wa wastani wa
asilimia 35 kwa mwaka. “Kwa mwaka 2019/2020, jumla ya miradi 304
inayohusiana na ujenzi wa viwanda imesajiliwa ambayo inatarajiwa
kuongeza jumla ya ajira 11,793.”
Amesema SIDO
imeratibu na kuhudumia viwanda vidogo vipya 1,400 vinavyotoa ajira
4,200. “Sekta hii muhimu imeajiri Watanzania zaidi ya milioni tisa ikiwa
ni ya pili kwa sekta za kiuchumi katika kutoa ajira baada ya sekta ya
kilimo,” ameongeza.
Amesema
maendeleo ya uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini yameongeza
uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za chuma, saruji, vigae,
nguo na mavazi, ngozi na bidhaa za ngozi, kusindika nyama, chakula,
mbogamboga na matunda, maziwa, mafuta ya kula, sukari, vifungashio,
mbolea, dawa za binadamu, sabuni na sigara pamoja na ubanguaji wa
korosho.
Kwa upande wa biashara, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa Blueprint for Regulatory Reform to Improve Business Environment umewezesha maboresho ya tozo 173 ambapo kati ya tozo hizo, tozo 163 zimefutwa na tozo kero 10 zimepunguzwa viwango.
“Kati ya tozo
zilizofutwa, 114 ni za sekta ya kilimo na mifugo, tano ni za Wakala wa
Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), 44 za Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Mamlaka za Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), utalii, maji, uvuvi
na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).”
Amesema tozo
zilizopunguzwa za GCLA, zimewezesha kuhamisha jukumu la usimamizi wa
masuala ya chakula kutoka iliyokuwa TFDA kwenda TBS ili kuondoa
muingiliano wa majukumu. “Maboresho hayo yamesaidia kuondoa urasimu na
kupunguza gharama za kufanya biashara,” amesisitiza.
Mapema, akimkaribisha
Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa maonesho hayo, Waziri wa Viwanda
na Biashara, Innocent Bashungwa alisema kati ya mwaka 2015 na 2019,
viwanda 8,477 vilianzishwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kati
ya hivyo, viwanda 201 ni vikubwa, 460 ni vya kati, 3,406 ni vidogo na
4,410 ni vidogo sana.
“Uwepo wa
viwanda vyetu vya ndani, ulitusaidia hata wakati wa janga la corona
tuliweza kutengeneza barakoa, mavazi ya watoa huduma, vitakasa mikono na
bidhaa nyingine nyingi.”
Akisisitiza
matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini, Waziri Bashungwa amesema:
“Hakuna soko endelevu na lenye uhakika kama soko la ndani. Kwa hiyo,
wazalishaji wa ndani wazalishe bidhaa zenye ubora, na Watanzania wapende
kununua bidhaa za ndani. Kwa njia hiyo, tutaimarisha soko la ndani na
kulinda viwanda vyetu,” alisisitiza.
Naye Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade, Dkt. Ngw’anza Kamata alisema
kutokana na changamoto ya COVID 19, mwaka huu idadi ya washiriki
imepungua kiasi. “Washiriki wa ndani wamepungua kutoka 3,250 hadi 2,837
wakati wa washiriki wa nje nao wamepungua kutoka 520 hadi 43,”
alisema.
No comments :
Post a Comment