……………………………………………………………
KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia PASCHAL MAYEGE [38] Mkazi wa Mkola Wilayani Chunya kwa
tuhuma za kumiliki silaha bunduki aina ya Gobole bila kuwa na
kibali.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako
uliofanyika tarehe 30.07.2020 majira ya saa 19:00 Jioni huko katika
Kitongoji na Kata ya Mkola, Tarafa ya Kipembawe,Wilaya ya Chunya, Mkoa
wa Mbeya. Mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo isiyokuwa na namba za
usajili ndani ya nyumba anayoishi. Upelelezi unaendelea.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA UVUNJAJI NA UPORAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linawashikilia watuhumiwa thelathini na moja [31] wote wanaume kwa
tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji, uporaji na vitendo
vingine vya uhalifu katika maeneo mbalimbali Jijini Mbeya.
Watuhumiwa wamekamatwa katika
misako iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi katika maeneo ya Nanenane,
Uyole, Uyole Kati, Itezi na Nyigamba katika vilabu vya pombe za kienyeji
wakinywa pombe huku wengine wakicheza kamali.
Aidha katika misako hiyo, zimekamatwa Pikipiki tatu [03] zinazodhaniwa kuwa ni mali za wizi ambazo ni:-
- MC.413 AQQ aina ya San lg.
- T.143 BTH aina ya Fekon.
- Pikipiki aina ya T-Better isiyo kuwa nan amba ya usajili.
Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linawashikilia watuhumiwa wanne 1. MPESSO NJAGAJA @ MOPOZE [40], 2.
MBALAMWEZI SASAJILA [42], 3. MAATON HAUS [51] na 4. LAMECK HAUS [60]
wote wakazi wa Ikukwa kwa tuhuma za mauaji ya ELIAS NZIYAJE @ MIYOMBE
[41] tingo wa lori la Mapembelo.
Watuhumiwa wamekamatwa mnamo
tarehe 02.07.2020 majira ya saa 02:00 usiku huko Kijiji na Kata ya
Ikukwa, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya baada ya kutafutwa kwa
muda mrefu kutokana na tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya
ELIAS NZIYAJE @ MIYOMBE [41] lililotokea mnamo tarehe 24/05/2020 huko
Kijiji na Kata ya Ikukwa, Wilaya ya Mbeya Vijijini. Upelelezi wa shauri
hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa
mahakamani.
MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia UPENDO ANYIMIKE MWANG’ONDA [48] Mkazi wa Ilima kwa tuhuma
za mauaji ya SINARAHA MWANG’ONDA [84] Mkazi wa Ilima.
Tukio hili limetokea tarehe
02.07.2020 majira ya saa 18:00 jioni huko Kijiji na Kata ya Ilima,
Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya ambapo SINARAHA
MWANG’ONDA [84] mkazi wa Ilima aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha
kali kichwani akiwa amelala nyumbani kwake.
Chanzo cha tukio hili ni tuhuma za
wizi kwani tarehe 01.07.2020 majira ya saa 13:00 Mchana marehemu
alituhumiwa kuiba Pipa mali ya UPENDO ANYIMIKE MWANG’ONDA alishitakiwa
kwa Balozi na aliamriwa alipe fedha taslimu kiasi cha Tshs.20,000/= kama
fidia lakini hakuonekana mpaka alipokutwa ameuawa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
AJALI YA MOTO NA KUSABABISHA KIFO.
Mnamo tarehe 02.07.2020 majira
ya saa 16:30 Jioni huko Kitongoji cha Jejere, Kijiji cha Mahongole,
Kata ya Imalilo Songwe, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa
Mbeya. Mtoto MASELE JOSEPH, miezi 04 na mkazi wa Mahongole alifariki
dunia baada ya kuungua moto akiwa amelazwa na mzazi wake katika kibanda
cha nyasi shambani.
Chanzo cha tukio ni uzembe wa
mzazi kutokuwa makini kwa mtoto wake PENDO JOSEPH miaka 04 aliyechoma
kibanda hicho kwa kibiriti wakati mzazi wake akiwa shambani. Mwili wa
marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali. Upelelezi
unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia MBESO NJANGAJE @ MWAMPOZIA [40] Mkazi wa Ikukwa katika
Halmashauri ya Mji Mdogo Mbalizi akiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi
yenye uzito wa kilo 10 na gramu 215.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe
02.07.2020 majira ya saa 02:00 Usiku huko Kitongoji cha Itende – Juu,
Kijiji na Kata ya Ikukwa, Tarafa ya Usongwe. Mtuhumiwa ni muuzaji na
mtumiaji wa bhangi na atafikishwa mahakamani leo tarehe 03.07.2020.
No comments :
Post a Comment