Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(katikati) akiwa pamoja na
viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Katavi wakikagua ujenzi wa kituo cha
Kupoza umeme cha Inyonga,kilichopo Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi,Julai
8,2020.
Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu,(aliyekaa) akipewa baraka na kiongozi wa kimila ya
kijiji cha Nsekwa, wakati alipokwenda kuwasha umeme kwenye kijiji hicho
Julai,8,2020.
Mafundi wakindelea na ujenzi wa cha kituo cha Kupoza umeme cha Inyonga, kilichopo Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi,Julai,8,2020.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akikata utepe kuashiria kuashwa
kwa umeme katika kijiji cha Nsekwa, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi,Julai
8,2020,kulia ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack
Kamwelwe, ambae pia ni mbunge wa jimbo la Katavi.
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(katikati) akikagua ujenzi wa kituo cha
Kupoza umeme cha Ipole, kilichopo Wilaya ya Sikonge,Mkoani
Tabora,Julai,8,2020.
****************************************
Hafsa Omar-Katavi, Tabora
Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu, Julai 8,2020 amefanya ziara ya ukaguzi wa
ujenzi ya
vituo vya kupoza umeme(substation) vilivyopo katika Mkoani
Katavi na Tabora.
Katika ziara yake
hiyo, ya Ukaguzi wa Mradi wa njia kuu ya kusafirisha umeme wa Gridi ya
Taifa kutoka Ipole Tabora hadi Mpanda Katavi,alikagua kituo cha Inyonga
kilichopo mkoani Katavi na kituo cha Ipole kilichopo mkoani Tabora.
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo,amesema ameridhishwa na
kasi ujenzi ya mradi huo ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka
huu, mradi ambao unatarajiwa kuazalisha takribani megawati 28 za awali.
Aidha, amewataka
wakandarasi wa mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha
mradi huo unamalizika kwa wakati ili kufanikisha lengo la mikoa hiyo
kuanza kutumia umeme wa Gridi ya Taifa.
“Mradi huu wa
kupeleka umeme wa gridi ya Taifa katika mkoa wa Katavi ni miongoni mwa
kipaumbele chetu kwakweli tutaendelea kusimamia mradi huu ili umalizike
kama ulivyopangwa,”alisema.
Pia, amesema
amefurahishwa kwa kupungua kwa gharama za ujenzi wa mradi ambao hapo
awali ulikuwa ugharimu kiasi cha shilingi bilioni 135 lakini kwasasa
utagharimu shilingi bilioni 70.
Vilevile,amelipongeza
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa usimamizi mzuri, na kuwataka
kuendelea kwa usimamizi wa ujenzi wa line ya kusafirishia umeme katika
mradi huo, na kuwataka kuendelea kutenga fedha kwaajili ya ujenzi huo
ili ukamilike kwa haraka.
Kwa upande wake,
Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Neema Mushi amesema,mara baada ya kupewa
maagizo ya kupeleka umeme wa gridi katika katika mkoa huo walianza kazi
hiyo mara moja ili kufanikisha lengo hilo,ambapo hadi sasa vituo vyote
vipo katika hatua ya ujenzi ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa
mwaka huu.
Pia, alisema
mradi huo utakapomalizika utazalisha megawati 28 za awali ambapo
kutakuwa na fida sita, ambazo mbili zitakuwa kwaajili ya matumizi ya
viwanda na nne kwaajili ya matumizi ya wananchi.
Awali, akiwa
mkoani Katavi, Naibu Waziri aliwasha umeme katika kijiji cha Nsekwa
kilichopo, wilaya ya Mlele na kuwataka wananchi wa kijiji kutokuwa na
wasiwasi kwasababu ujenzi wa kituo cha kuupoza umeme unatarajiwa
kumalizika mwishoni mwa mwaka huu na waakazi wa Katavi watapata umeme wa
uhakika.
No comments :
Post a Comment