*******************
VICTOR MASANGU, PWANI … HABARI ..MAUAJI YA KIKATILI
WATU watatu
wamefariki dunia wakiwiwemo watoto wawili wa familia moja ambao ni
wanafunzi wa shule ya msingi Kwazoka kuuwawa kikatili baada ya
kukatwa katwa na mapanga na mfanyakazi wa kazi wa ndani wa kiume
aliyetambulika kwa jina la Yasin Abdalah mwenye umri wa miaka 35 kisha
na yeye kuuliwa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza na
waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Mwakyo Nyigesa amesema tukilo hilo limetokea jana majira ya saa moja
usiku katika kitongoji cha Kivungwi Kazoka Kata ya Vingwaza kilichopo
Wilayani Bagamoyo.
Katika hatua
nyingine Kamanda Nyigesa amewataka wananchi Mkoa wa Pwani kuachana
kabisa na tabia ya kujichukulia sheria mikononi na kwamaba miili ya
marehemu hao watatu imehifadhiwa katika Kituo cha afya Mlandizi
kilichopo Wilayani Kibaha na kuongeza kwamba mtuhumiwa huyo kabla ya
umauti wake alivunja mlango wa ofisi za kijiji na kukimbia alipokuwa
amehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake.
No comments :
Post a Comment