Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny
Mwaipaja, (wa pili kushoto) akiwaongoza wawakilishi wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara hiyo kumkaribisha Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za
Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti, alipofika kujionea huduma na elimu
inayotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja
wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti, akisaini
kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na
Mipango katika Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara jijini Dar es
salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bi. Josephine Majura.
Kamishna
Msaidizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha
na Mipango, Bi. Dionisia Mjema, akimuongoza Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa
nchi za Afrika Mashariki Mhe. Manfredo Fanti, kutembelea na kupata
maelezo mbalimbali ya huduma na elimu inayotolewa na wizara hiyo pamoja
na Taasisi zake wakati balozi huyo alipotembelea Maonesho ya 44 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango
wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Bw. David Magabe, akitoa
ufafanuzi kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki
Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu namna Serikali, Mashirika ya Umma na
Kampuni Binafsi zinavyoweza kupata mitaji ya kugharamia miradi ya
maendeleo kupitia masoko ya mitaji, wakati balozi huyo alipotembelea
banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika
Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar Es
Salaam.
Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango , Bw.
Benny Mwaipaja, akimkabidhi Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika
Mashariki Mhe. Manfredo Fanti machapisho mbalimbali ya wizara hiyo
wakati balozi huyo alipotembelea banda la wizara katika Maonesho ya 44
ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments :
Post a Comment