Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi
na Bulyanhulu, Benedict Busunzu (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya
Kahama, Mhe. Anamringi Macha hundi ya shilingi 1,159,817,107.83/=
zilizotolewa na Mgodi wa Buzwagi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama ikiwa
ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi
Juni 2020. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama,
Underson Msumba. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe.
Anamringi Macha (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji
Kahama, Underson Msumba hundi ya shilingi shilingi 1,159,817,107.83/=
zilizotolewa na Mgodi wa Buzwagi kwa halmashauri ya Msalala ikiwa ni
malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi
Juni 2020.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi
na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama,
Mhe. Anamringi Macha hundi ya shilingi shilingi 376,004,787.02/=
zilizotolewa na Mgodi wa Bulyanhulu kwa halmashauri ya Msalala ikiwa ni
malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi
Juni 2020. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon
Berege.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi
na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5
(1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji
ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi
Januari hadi Juni 2020 zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya
Twiga Minerals Corporation.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi
na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5
(1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji
ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi
Januari hadi Juni 2020 zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya
Twiga Minerals Corporation.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi
na Bulyanhulu, Benedict Busunzu akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5
(1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji
ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi
Januari hadi Juni 2020 zilizotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya
Twiga Minerals Corporation.
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya
Kahama, Joachim Simbila akiipongeza Kampuni ya Twiga Minerals kwa kulipa
ushuru na kuziomba halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia vizuri
fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi iliyokusudiwa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe.
Anamringi Macha akizungumza wakati Kampuni ya uchimbaji madini ya Twiga
Minerals Corporation kupitia migodi yake ya dhahabu ya Buzwagi na
Bulyanhulu ikikabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5
(1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya Msalala na Kahama Mji
ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia mwezi
Januari hadi Juni 2020.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe.
Anamringi Macha akiziagiza halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia
fedha hizo kwa utaratibu utakaoleta tija kwa wananchi.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kampuni
ya uchimbaji madini ya Twiga Minerals Corporation kupitia migodi yake
ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu imekabidhi hundi zenye thamani ya
shilingi Bilioni 1.5 (1,535,821,894.85/=) kwa halmashauri ya wilaya ya
Msalala na Kahama Mji ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi
cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2020.
Akikabidhi hundi hizo kwa Mkuu
wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha leo Jumatano Julai
15,2020,Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Busunzu
amesema lengo la migodi hiyo ni kuona mamlaka husika zinaelekeza fedha
hizo katika miradi inayolenga kuwaletea maendeleo wananchi wanaozunguka
migodi.
Busunzu alifafanua kuwa mgodi wa
Buzwagi umelipa shilingi 1,159,817,107.83/= kwa halmashauri ya Mji wa
Kahama huku mgodi wa Bulyanhulu ukilipa shilingi 376,004,787.02/= kwa
halmashauri ya wilaya ya Msalala.
“Migodi ya Twiga Minerals
chini ya Kampuni ya Barrick nchini Tanzania hulipa ushuru wa huduma kila
baada ya miezi sita kwa halmashauri ili ambazo migodi yetu inaendesha
shughuli zake kulingana na mapato ya kila mwaka ambapo malipo haya ni
kutekeleza hitaji la kisheria na ni sehemu ya mikataba ya makubaliano
kati ya migodi na halmashauri husika”,aliongeza Busunzu.
“Tunatoa ushuru ili kuboresha
utoaji wa huduma katika jamii zinazozunguka migodi katika sekta
mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu,afya na upatikanaji wa maji safi na
salama”,alisema.
Aidha alisema licha ya migodi
hiyo kulipa kodi stahiki bado imekuwa ikijishughulisha katika
kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa maendeleo kupitia sera yake ya
maendeleo ya jamii ni kuwa ikiwa ni kuunda fursa endelevu za kiuchumi na
maendeleo kwa katika jamii na kuinua uchumi wa wilaya na kuboresha
ustawi wa maisha ya wenyeji.
Akipokea hundi hizo, Mkuu wa
wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha aliipongeza kampuni ya Twiga
Minerals kwa kutoa ushuru wa huduma ikiwa ni zao la kwanza chini ya
Twiga iliyotokana na ubia kati ya serikali na Barrick huku akiziagiza
halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia fedha hizo kwa utaratibu
utakaoleta tija kwa wananchi.
“Sisi tunataka fedha zinaenda
kwenye miradi ambayo itakuwa na tija kwa ajili ya maendeleo ya vijana,
watu wenye ulemavu,wanawake. Mkono wa serikali bado upo pale pale
kuhakikisha fedha hizi zinakwenda kutekeleza ile miradi tuliyoikusudia”,alisema Macha.
Alisema fedha hizo zitatumika
kutekeleza miradi ya maendeleo katika jamii ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika
sekta ya elimu,afya,maji na miradi mingine itakayogusa wananchi moja kwa
moja.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya
Kahama, Joachim Simbila aliipongeza Kampuni ya Twiga Minerals kwa kulipa
ushuru huku akiziomba halmashauri za Msalala na Kahama Mji kutumia
vizuri fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi iliyokusudiwa.
No comments :
Post a Comment