Na, Woinde Shizza michuzi Tv, ARUSHA
WAHITIMU wa kidato cha sita mwaka huu wenye ndoto za kusoma Elimu
ya juu Nje ya Nchi, wamepata auhueni kwa kupatiwa mkopo wa Elimu ya Juu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Meneja Mkuu wa
kampuni ya Global Education Link(GEL) Regina Lema, alisema kumekua na
changamoto ya kifedha kwa wanafunzi wanaosoma nje ya Nchi hivyo wao
wameamua kuitatu.
Aidha alibainisha kuwa, GEL, kama mawakala wa Vyuo vikuu nje ya nchi,
wameamua kutoa Mikopo hiyo ya Elimu ya juu kwa kushirikiana na Mwalimu
Commercial Bank pamoja na Amana Bank, ili kusaidia wepesi wa wanafunzi
kusoma bila wasiwasi wawapo nje ya Nchi.
"Tumeshuhudia serikali ikiwapa mkopo wanafunzi wa hapa
nyumbani(Tanzania) mkopo wa Elimu ya juu kila mwaka, Tumekaa tukawaza,
hawa wengine wanaosoma nje ya Nchi wao aanasaidikaje, Sasa tumeona ni
bora nao tuwakumbuke, na sisi kama taasisi ya uwakala wa wanafunzi nje
ya Nchi, kwakushirikiana na MCB, Na Amana Bank tuwape wanafunzi Wetu
mkopo huu ambao utafanyiwa mchakato ndani ya saa 48 Tu" Alisema Regina
Hata hivyo alisema kua kwa sasa taasisi ya GEL ina matawi katika
Kanda zote Tanzania, Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya Na
Zanzibar, hivyo huduma hiyo itawafikia vijana wote, waliomaliza kidato
cha sita ama diploma na wana ndoto za kusoma ama kujiendeleza katika
Elimu ya juu nje ya nchi kwa urahisi.
Global education link ni wakala wa Vyuo vikuu nje ya Nchi,
anaetambulika na Tume ya Vyuo vikuu Nchini (TCU)ambao wanahusika
kuwaunganisha wanafunzi na vyuo vikuu zaidi ya 200 Duniani kwa ajili ya
Elimu ya juu.
No comments :
Post a Comment