Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na
Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) pamoja na
Wajumbe alipokuwa akifunga mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akisistiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika
jana Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akifunga mkutano wa baraza
kuu la shirikisho hilo.
Rais wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza
jambo wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Shirikisho hilo uliofanyika
Mkoani Morogoro.
Kaimu Msaijili wa Vyama vya
Wafanyakazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Pendo Berege (kushoto)
akifuatilia mkutano huo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw.Heri Mkunda.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akifurahia jambo wakati wa
mkutano huo. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
nchini (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokya.
Sehemu ya Wajumbe Wanawake wa
shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) wakiburudika na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama (kulia) akikabidhiwa Katiba ya Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi nchini (TUCTA) na Rais wa Shirikisho hilo, Bw. Tumaini
Nyamhokya (katikati). Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Said Wamba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akiwa ameambatana na Viongozi wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) mara baada ya kuwasili katika mkutano
huo wa Baraza kuu. Kushoto ni Rais wa Shirikisho hilo, Bw. Tumaini
Nyamhokya.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) pamoja na Uongozi wa Chama
cha Walimu (CWT).
………………………………………………………………………………….
Na; Mwandishi Wetu, Morogoro
Ushirikiano mzuri
baina ya Serikali na Wafanyakazi umechangia katika kuifanya Tanzania
kuwa
miongoni mwa nchi iliyofikia uchumi wa kati mwaka huu 2020.
Hayo yameelezwa
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa
akifunga Mkutano wa Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(TUCTA) uliofanyika Mkoani Morogoro.
Waziri Mhagama
alieleza kuwa bidii ambayo wafanyakazi nchini wameonesha katika
utekelezaji wa majukumu yao kwenye sekta mbalimbali imekuwa ni chachu
kwa taifa katika kufikia uchumi huo wa kati mapema sana wakati ilikuwa
imelenga kufikia kiwango hicho 2025.
“Hali ya ukuaji
wa uchumi hadi hapa ilipofikia ni kutokana na Serikali ilivyoweza
kutekeleza kazi yake kwa kushirikiana na wafanyakazi ambao wamekuwa ni
msingi mkubwa wa maendeleo ya uchumi wa nchi,” alieleza Mhagama
“Hii ni ishara
kuwa Wafanyakazi wamekuwa na ushirikiano wa karibu na serikali yao na
pia wameonyesha dhamira dhati na utayari wa kujitolea kushiriki kwenye
sekta mbalimbali za kimaendeleo ambazo zitaboresha Maisha ya watanzania
kwa ujumla,” alisema Mhagama
Alifafanua
kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
mageuzi makubwa sana ya kiuchumi, akitolea mfano wa jitihada kumbwa
alizozifanya ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati pamoja
na jinsi anavyosimamia sera za uchumi nchini ambazo leo hii tunashuhudia
maendeleo yaliyopo nchini.
“Mheshimiwa Rais
aliwapongoza wananchi kwa mafanikio hayo ila kipekee pia tatambue na
kupongeza juhudi zake katika kuiwezesha Tanzania kuingia uchumi wa
kipato cha kati,” alisema Mhagama
Alieleza kuwa
Shirikisho hilo ni chombo muhimu kinachowaunganisha wafanyakazi wote
nchini na ndio kinachofanya kazi na serikali katika kuhakikisha haki na
majukumu ya wafanyakazi yanawasilishwa Serikalini na kwa waajiri
nchini.
Aliongeza kwa
kuwapongeza wafanyakazi nchini kuwa sehemu ya mafanikio hayo ambayo
yataweza kuboresha hali zao ikiwemo maslahi ya wafanyakazi.
“Serikali
itaendelea kuthamini mchango wa Vyama vya Wafanyakazi katika kuimarisha
mshikamano na umoja kwa kuheshimu dhhana ya utatu,” alisema
Sambamba na hayo
amelitaka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kutengeneza mpango
kazi wa kutoa elimu ya Sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya ajira na
mahusiano kazini kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
“Nimatumaini
yangu mkiwa na mpango huo utawasaidia kupata elimu itakayo wawezesha
kuwa na majadiliano mazuri baina ya waajiri na wafanyakazi, na itakuwa
ni suluhisho ya kutatua migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza,” alisema
Mhagama
Alieleza, Ofisi
ya Waziri imeandaa programu maalumu inayolenga kuvifikia vyama vyote vya
wafanyakazi lengo ikiwa ni kuwapatia ujuzi wa masuala mbalimbali
kuhusiana na sekta hiyo ya kazi ikiwemo namna ya kuandaa mikataba ya
hali bora ambayo imekuwa ni chachu kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu
yao kwa ufanisi.
Aidha, Waziri
Mhagama ametoa maagizo kwa Viongozi wa TUCTA pamoja na Vyama vya
Wafanyakazi vyote kwa ujumla kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya matumizi
ya fedha na rasilimali za vyama vyao, kuheshimu maamuzi ya vikao na pia
maamuzi yatakayotolewa na viongozi yawe shirikishi, kupunguza mogogoro
isiyo ya lazima pamoja na kuwasisitiza wanapoelekea kwenye uchaguzi wa
vyama vyao wafuate taratibu na kuzingatia sheria na kanuni.
Kwa Upande wake,
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini
Nyamhokya aliahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na alielezea
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli imekuwa ikishirikiana na Vyama vya Wafanyakazi kwa karibu
pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali ya wafanyakazi.
“Serikali hii ya
awamu ya tano imetufanyia mambo mengi wafanyakazi, katika kipindi hiki
suala la punguzo la kodi kwa wafanyakazi limekuwa ni faraja kubwa kwa
wafanyakazi, tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali kutokana na
namna inavyotujali,” alisema Nyamhokya
Naye Kaimu Katibu
Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Said Wamba alisema
kuwa Shirikisho hilo la Vyama vya Wafanyakazi litaendelea kudumisha
mshikamono na umoja kwa kutetea maslahi ya wafanyakazi ili waweze
kufanyakazi kwa tija na kuleta ufanisi kwenye sekta ya kazi.
Mkutano huo wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ulianza rasmi 29
Juni 2020 na kuhitimishwa Julai 3, 2020 ambapo katika mkutano huo
yalitolewa mafunzo kwa viongozi na wajumbe kutoka kwenye vyama shiriki
13 ikiwemo CWT, TUICO, TALGWU, TUICO, TUGHE, CHODAWU, TEWUTA, TPAWU,
TAMICO, COTWU (T), DOWUTA, RAAWU, TRAWU na TASU.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
OWM – KVAU
No comments :
Post a Comment