*****************************
Bilionea wa Tanzanite, Laizer
Saniniu leo Julai 12 , 2020 ametembelea mabanda mbalimbali kwenye
Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza akiwa kwenye mabanda
hayo amewataka wachimbaji madini wadogo wadogo
wasibweteke na fedha
kidogo wanazopata na kuwafanya waache kuendelea kuchimba madini na
badala yake wanatakiwa kuendeleza jitihada za kuchimba na ipo siku
wataibuka mabilionea
Laizer akifafanua zaidi mbele ya
waandishi wa habari katika banda la Tume ya Madini amesema kwamba “Mimi
nimetokea familia ya hali ya chini, nimekuwa mvumilivu sana katika kazi
hii ya uchimbaji madini.
“Sikukata tamaa kwa fedha ndogo
ndogo nilizokuwa napata kutokana na uchimbaji, niliendelea kuchimba
nikiamini ipo siku Mungu atanipatia mawe ya kunipa kipato kikibwa zaidi
na kweli ndivyo ilivyokuwa.”
Ametumia nafasi hiyo kuishukuru
Serikali kwa kila hatua waliyochukua kwa ajili ya mchakato wa kupima
madini yake na kisha kuyanunua na kumpatia fedha hizo kwa uaminifu.
Hata hivyo ameziomba mamlaka
husika zisiwanyaanyase wachimbaji wadogo kwani wengi wao ni masikini
sana na wanategemea kazi hiyo iweze kuwainua kiuchumi pamoja na familia
zao.
No comments :
Post a Comment