Wednesday, July 15, 2020

Airtel yazindua ONGEA BURE kwa kila muamala wa Airtel Money



Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda pamoja na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando wakionyesha bango ikiwa ni uzinduzi wa ofa mpya na kabambe ambapo sasa wateja  wataweza kuongea BURE kila wanakapofanya muamala wowote kupitia Airtel Money. Miamala itakayomuweza mteja wa Airtel Money kufurahia ofa ya ONGEA BURE ni pamoja na kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipa bili, kununua bando au muda wa maongezi.
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda pamoja na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando wakionyesha bango ikiwa ni uzinduzi wa ofa mpya na kabambe ambapo sasa wateja  wataweza kuongea BURE kila wanakapofanya muamala wowote kupitia Airtel Money. Miamala itakayomuweza mteja wa Airtel Money kufurahia ofa ya ONGEA BURE ni pamoja na kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipa bili, kununua bando au muda wa maongezi.
Airtel yaja na Unafuu palepale kwa watumiaji wa Airtel Money
Dar es Salaam Jumatano 15 Julai 2020; Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imeendelea kudhihirisha ubunifu katika kutoa huduma bora kwa kutoa unafuu zaidi kwa wateja wake wanaotumia  huduma ya Airtel Money kwa  kuja na kampeni kabambe ambapo sasa wateja  wataweza kuongea BURE kila wanakapofanya muamala wowote kupitia Airtel Money.
Miamala itakayomuweza mteja wa Airtel Money kufurahia ofa ya ONGEA BURE ni pamoja na kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipa bili, kununua bando au muda wa maongezi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo na waandishi wa habari wakati wa kuitambulisha rasmi ofa mpya ya ONGEA BURE kila unapofanya Muamala kupitia Airtel Money, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema “Airtel Tanzania imeamua leo kuzindua kampeni hii  kabambe ya fanya muamala kwa Airtel Money ujipatie dakika za muda wa maongezi BURE kuendelea kudhihirisha ile dhamira  yetu ya unafuu pale pale ili wateja wetu wote kuendelea kuziamini na kuzitumia huduma zetu za Airtel Money wakati wowote watakapotaka kulipia  huduma na bidhaa mbali mbali kila siku”.
 ‘Huduma ya Airtel Money ni kati ya huduma bora za fedha kwa njia ya mtandao inayokuwa na kwa kasi sana  hapa nchini ambapo kwa sasa ina  zaidi ya watumiaji milioni tano, mawakala walioenea nchini kote zaidi ya 100,000 na maduka ya huduma kwa wateja yaani Airtel Money branches zaidi ya 1,500. Tunajivunia kuwa na wigo mpana wa maduka na huduma bora za  Airtel Money kwa upanukaji  wa harakana  unaofikia lengo letu la  kufikisha huduma  maeneo ya  vijijini na miji mikuu”. Alisema Nchunda huku akitoa rai kwa Watanzania kuendelea kutumia huduma ya Airtel Money kwani ni haraka, nafuu na salama.
Nchunda alieleza kuwa “ofa ya 'ONGEA BURE’ kila ukifanya muamala kwa Airtel Money inalenga kuimarisha njia za kisasa za malipo kwa njia ya mtandao badala ya kutegemea malipo ya pesa taslimu ambayo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya sasa. Alisema ili mteja kufaidika na ofa ya ONGEA BURE, “fanya muamala kwa Airtel Money kwa kupiga*150*60# kupata menyu ya Airtel Money unayoihitaji ikiwa ni kutuma pesa, kununua muda wa maongezi au bando, kutoa pesa kwa wakala yeyote na papo hapo atapokea ujumbe mfupi wa maneno wa kwamba umejipatia muda wa maongezi sasa Ongea BURE”.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa “Airtel Tunaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuwa suluhisho kwa sekta ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kwa kuzindua huduma ambazo ni nafuu zaidi, zinazopatikana kwa urahisi na salama, huku tukiendelea kuwazawandia wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma za Airtel Money. Vile vile, mpango wetu unaoendelea wa upanuzi wa mtandao wetu ni moja ya mkakati wa kampuni yetu kutoa suluhisho la huduma za mtandao ndani ya nchi na hata na kimataifa.
 “Mpango wetu ni kuendelea kuunda mtandao madhubuti na wa kutengemewa na watanzania wengi.  Piga *150*60# kupata OFA hii ukiwa popote au kwa tembelea Airtel Money Branches zetu na kupata huduma zaidi kama vile kutoa na kuweka pesa, kurudisha muamala uliokosewa, kubadilisha PIN pamoja na kusajili laini mpya kwa alama za vidole”.  alisema Singano.

No comments :

Post a Comment