Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (kwanza
kushoto) akimsikiliza Meneja wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Alban Kihulla
mara baada ya kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa
Pwani kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya. Pichani ni mashine ya
kupima dira za maji zinazotumiwa taasisi zinazotoa huduma za maji.
Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/Michuzi Tv
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (kwanza
kulia) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu-WMA, Dkt. Ludovick
Manege (katikati) mara baada ya kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo
Misugusugu Mkoa wa Pwani kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (wa pili
toka kushoto) akiangalia jinsi shughuli za upimaji wa matanki ya mafuta
unavyofanyika.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (kwanza
kushoto) akimsikiliza Meneja wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Alban Kihulla mara
baada ya kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani
kujionea shughuli mbalimbali wanazofanywa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe
akizungushwa sehemu mbai mbalimbali za jengo na Afisa Mtendaji Mkuu-WMA,
Dkt.Ludovick Manege.
Afisa Mtendaji Mkuu-WMA, Dkt.Ludovick Manege akifafanua jambo kwa wanahabari Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani.
Katibu
Mkuu wa Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumaliza ziara yake katika kituo cha Wakala wa
Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi Tv.
Kwasasa
wamekuwa wakipima magari ya mafuta na dira za maji lakini kwa kufikia
mwezi wa kumi watakuwa wameshaanza kupima dira za umeme kwasababu tayari
taratibu za manunuzi zimekamilika.
Kauli
hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu -WMA, Dkt. Ludovick Manege wakati
akitoa maelezo machache kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara
Prof. Riziki Shemdoe mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo
Misugusugu Mkoa wa Pwani.
Dkt.
Manege amesema kuwa utaratibu wa kuwepo kwa mtambo wa kupima mita za
umeme ulikwishaanza na kufikia mwishoni mwa mwaka huu utakuwa tayari
umeshakamilika.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki
Shemdoe mara baada ya kutembelea kituo hicho amewataka WMA washirikiane
na Tanesco pamoja na TPDC ili kuweza kufanikisha jambo la kupima mita
zinazoweza kutumika katika matumizi.
“WMA
wameanza mkakati wa kupima mita za umeme, niombe suala hili lifanyiwe
kazi kwa haraka lile jengo ambalo linatakiwa lijengwe kwa ajili ya
kuhifadhi mtambo wa kupima mita za umeme lijenge na ikiwezekani kabla ya
mwisho wa mwaka huu”. Amesema Prof. Shemdoe.
Aidha
Prof. Shemdoe ameomba kuanza mchakato wa kupata mtambo mwingine ambao
utasaidia kupima mita za gesi zinazotumika viwandani na pengine ambazo
tumeanza kuzitumia majumbani ili waweze kulipa kutokana na matumizi
sahihi.
No comments :
Post a Comment