Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe
ameeleza kuwa lengo la kuihamisha Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA) kutoka
Wizara ya Viwanda na Biashara kuja katika Wizara anayoisisimamia ni
kuhakikisha wadau wa Sanaa wanapata huduma sehemu moja kwa sababu
asilimia 86% ya wadau wake ni Wasanii.
Dkt.
Mwakyembe ameyasema hayo jana Jijini Dodoma katika Mkutano na Waandishi
wa habari ambapo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli jana tarehe 13/07/2020 amesaini Waraka unaogawa
majukumu kwa wizara kuruhusu mabadiliko hayo muhimu ambayo yanawagusa
wabunifu,watunzi waandishi wa vitabu,kazi za Sanaa na Sanaa na jadi.
“Namuagiza
Katibu Mkuu wa Wizara hii ndani ya saa ishirini na nne awe amekutana na
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ili waweze kukabidhiana
nyaraka muhimu za uendeshaji wa COSOTA”alisema Dkt.Mwakyembe.
Aidha
Waziri huyo ameeleza kuwa ujio wa COSOTA katika Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo utarahisisha ushirikiano na Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA) katika kulinda na kusimamia maslahi ya
wasanii wa filamu na muziki pamoja na kupanua wigo wa malipo na stahili
za wasanii kwa kazi zao katika majukwaa mbalimbali ya Sanaa
kielektroniki.
Mhe.Waziri
amesisitiza kuwa lazima COSOTA ya sasa iingie mikataba na nchi za nje
ambazo vyombo vyake vya habari vimekua vikipiga muziki wa wasanii wa
Tanzania bila kuwapatia gawio au kufaidika kwa namna yoyote ile.
…MWISHO..
No comments :
Post a Comment