Wanafunzi
wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Tumaini iliyopo
wilayani Iramba mkoani Singida wakifurahia kupata bomba la maji kwa
ajili ya kutakasa mikono ili kujikinga na Covid 19 lililo jengwa na
Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA)
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo (kulia) akika utepe kuashiria
uzinduzi wa bomba la maji lililojengwa na wizara hiyo kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA) kwa
ajili ya kujikinga na ugonjwa wa Corona katika Shule ya Sekondari ya
Tumaini iliyopo Iramba mkoani Singida mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo (kulia) akimkabidhi dawa ya kutakasa mikono Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA) Mhandisi Patrick Nzamba,
Bomba la maji lililozinduliwa shuleni hapo.
Mkuu wa shule hiyo, Honoratha Ndiaji alishukuru kwa shule hiyo kupata msaada huo.
Wanafunzi wakifurahia msaada huo.
.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
WIZARA ya
Maji katika mwaka wa fedha ujao itatenga Sh.Bilioni 2 kwa ajili ya
kupeleka huduma ya maji kwenye mashule na vituo vya afya.
Hayo
yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo
wakati akizindua bomba la maji lililojengwa na wizara hiyo kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida
(SUWASA) kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa Corona katika Shule ya
Sekondari ya Tumaini iliyopo Iramba mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
Mkumbo
alisema wizara hiyo mwaka huu wa 2020/ 2021 wameanzisha programu maalumu
ya kupeleka huduna za jamii kwenye taasisi za za kijamii kwa maana
vituo vya afya na shule za sekondari na msingi.
”
Tunachokifanya leo hapa ni kutoa alama mbili, alama ya kwanza ni
kuonesha mwaka unaokuja tunakwenda kutekeleza programu ya kupeleka maji
kwenye taasisi zetu.Lakini ya pili ni kama alivyoagiza Rais wetu Dk.John
Magufuli shule zetu zifunguliwe huku tahadhari ya kujikinga na na
Corona hivyo tuliwaelekeza wataalamu wetu wasaidie kutengeneza
miundombinu ya kunawa mikono kwa sabuni na sisi tutatoa mchango wa maji
na Halmashauri zitoe sabuni.” alisema Mkumbo.
Alisema
kwa Mkoa wa Singida waliichagua shule kongwe ya Tumaini na pia mtu huwa
haachi nyumbani kwao kwa vile na yeye anatoka eneo hilo akaona ni vizuri
msaada huo ukapelekwe kwenye shule hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa SUWASA Mjini Singida, Mhandisi Patrick Nzamba alisema
wamejipanga kuhakikisha wanajenga miundombinu ya kutoa maji.
Alisema
sambamba na hilo wameweza kuweka vituo vya kunawia sehemu mbalimbali
katika Manispaa ya Singida, Soko la Kimataifa la Vitunguu, Stendi ya
Mabasi na sasa katika shule hiyo.
Mkuu wa
Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula alisema msaada huo katika shule hiyo
ni wa kizalendo hivyo akatoa rai ya kuhimiza miundombinu kutunzwa.
Mkuu wa shule hiyo, Honoratha Ndiaji alishukuru kwa kusema kuwa msaada huo kwao ni faraja kubwa.
Kwa
upande wake Mwanafunzi wa Kidato cha Sita katika shule hiyo, Alice
Katunzi alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuruhusu kidato cha sita
kuendelea na masomo hivyo wamemuahidi watahakikisha wanafunzi wote
wakidato hicho nchi nzima wanapata alama A.
No comments :
Post a Comment