Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi msimu
wa Kahawa wa mwaka 2020/2021 ikiwa ni pamoja na kutangaza bei ya
malipo ya awali shilingi 1200 kila kilo ya kahawa ya maganda kwa Vyama
Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 Limited, KDCU Limited na Ngara Farmers.
Mkuu
wa Mkoa Gaguti akitangaza ufunguzi wa msimu katika Chama cha Msingi
cha Mabira Wilayani Kyerwa Juni 9, 2020 alisema kuwa jukumu kuu la
Serikali ni kuhakikisha mkulima analindwa haki zake asipunjwe katika
bei pia muda wa kupata malipo yake uwe mfupi kutoka wiki moja hadi
masaa 48 tangu mkulima kufikisha kahawa yake katika Chama cha Msingi.
Gaguti
amewataka wafanya biashara ya kahawa ambao wapo tayari kununua kahawa
ya wakulima wa kahawa katika mkoa huo kuhakikisha wanafanya biashara
hiyo mchana kweupe bila kuwahujumu wakulima kwakuwa kahawa na biashara
halali na hakuna sababu ya kuuzwa gizani.
“Niwaombe
wafanyabiashara wenye nia ya kunua kahawa yetu fanyeni biashara hii
mchana kweupe maana hata wakulima wanavuna mchana kweupe, nielekeze tu
katika mkoa wa Kagera sitaruhusu biashara ya kahawa kufanyika usiku hii
sio biashara haramu” Alisisitiza Mkuu wa mkoa Gaguti.
Mkuu
wa Mkoa Gaguti alitumia fursa hiyo kurudia kauli yake kuwa kama kuna
mfanyabaiashara yeyote ambaye yupo tayari kununua kahawa kwa wakulima
kwa bei nzuri ajitokeze na kutangaza bei yake ili akapatiwe kahawa.
“Kufikia
tarehe 8.06.2020 tumepokea maombi ya wafanyabiashara wanane na kati ya
hao wawili tu waliwasilisha maombi kwa barua na mmoja ndiye aliomba
kununua kahawa kwa shilingi 1100 tu.” Alieleza Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia alitoa rai kwa wakulima kuhakikisha wanatunza ubora wa
kahawa yao kabla ya kuipeleka katika Vyama vya Msingi ili kuhakikisha
kahawa kutoka Mkoani Kagera inafika kwenye soko ikiwa na ubora
unaotakiwa ambapo katika msimu huu 2020/2021 zinatarajiwa kukusanywa
takribani kilo milioni 60 juu ya kiasi cha msimu uliopita ambapo
zilikusanywa kilo milioni 52.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw.
Japhet Justine katika hafla hiyo ya ufunguzi wa msimu wa kahawa mwaka
2020/2021 alisema kuwa Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vimekuwa
viaminifu tangu mwaka 2018 benki ya TADB ilipoanza kuvipa mkopo ambapo
msimu wa mwaka 2018 Benki hiyo ilitoa bilioni 30 na zililipwa zote,
msimu 2019 Benki ilitoa bilioni 23 na zote zililipwa.
“Aidha,
msimu huu wa 2020/2021 tayari tumeweka shilingi bilioni 7.7 katika
akaunti za Vyama Vikuu vya KDCU Limited na KCU 1990 Limited kwaajili ya
kukusanya kahawa ya wakulima na bila kuchelewesha malipo yao. Ndiyo
maana baada ya kuona uaminifu wa vyama hivyo vikuu tumeamua kupunguza
riba kutoka asilimia 12 na mwaka huu tunatoa mkopo kwa asilimia tisa tu
(9%).” Alifafanua Bw. Japhet
Kuanzia
Juni 9, 2020 wakulima wa zao la kahawa Mkoani Kagera wanahamasishwa
kuanza kukusanya kahawa katika Vyama vyao vya Msingi na fedha ya malipo
ya awali ipo tayari kwaajili ya kuwalipa.
No comments :
Post a Comment