Na WAMJW- Arusha.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin
Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini
Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili
kusikiliza changamoto zinazowakumba.
Dkt.
Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa
changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho
Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na
virusi vya Corona.
Dkt.
Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa
itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto
wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga.
“Nimekuja
kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu
kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa ”
alisema.
Aidha,
Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa
salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John
Pombe Magufuli na kusema anawapenda sana.
Mbali
na hayo Dkt. Mollel alisema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika
mpaka wa Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya
moja, huku akiweka wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na
uchumi baina ya nchi hizo.
Nae,
dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya Bw. Abdullah Hassan amesema
kuwa, kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka
Kenya kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na
ugonjwa wa Corona jambo ambalo sio kweli.
“Tunaishi
maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha
zaidi, sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili.
Kwa
upande wake, Japhet Jeremiah alisema kuwa, wamekuwa wakiombwa kiasi cha
shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, hali
aliyeweka wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania.
“Sisi
kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tumeambiwa tuna Corona, na mimi wiki
mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina
Corona na sijawai tumia dawa yoyote mpaka sasahivi” alisema
No comments :
Post a Comment