Serikali
imekutana na wadau wa zao la shahiri na zabibu kwa lengo la kurejesha
zao la shahiri na kutatua changamoto zilizopo katika sekta ndogo ya
Zabibu ili kuweza kukuza soko la mazao hayo na kuinua kipato cha
wakulima wake.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe katika
Mkutano uliyohudhuriwa na wanunuzi wa zao la zabibu na shahiri pamoja
na wakulima wa mazao hayo.
Aidha
Mhe. Bashe amesema kuwa kwa sasa wakulima wa shahiri hawana soko, hivyo
ni vyema kwa msimu ujao wakulima walime zao la shahiri.
Mhe.
Bashe ameuagiza uongozi wa kiwanda cha Tanzania Breweries (TBL)
kufunguliwaa au kukikodisha kiwanda cha Kilimanjaro ambacho kipo
mikononi mwao ili kianze kazi mara moja.
“Lengo
ni kutaka wakulima waweze kulima kwa msimu ujao na sisi serikali
tutahakikisha mikataba inakuwa sawa kwa pande zote mbili kwa mnunuzi na
mkulima na uwazi wa mikataba hiyo ili kila mmoja kunufahika katika zao
hilo”, ameeleza Mhe. Bashe.
Hata
hivyo katika mkutano huo Mhe. Bashe amewataka wakuu wa wilaya, wakuu wa
mkoa na warajis wa vyama vya ushirika watakapo saini mikataba hiyo na
Serikali ishirikishwe kikamirifu ili kulinda maslahi ya mkulima na
wanunuzi.
Kwa
zao la zabibu Mhe.Bashe amesema msimu wa kilimo unaanza mwezi wa nane
hivyo Serikali inahitaji uhakika wa masoko na wanunuzi wanatakiwa kusema
namna ambavyo watanunua zao la zabibu .
“Hatutaki
wakulima wa zabibu mwezi wa nane wakati wa kuvuna wapate shida ya
masoko na nahitaji kujua kwa mwezi huo tutavuna kiasi gani . Njia pekee
itakayotusaidia ni kuingia mkataba na wakulima” ameweka wazi Mhe. Bashe.
Kwa
kuongezea Mhe. Bashe ametoa wito kwa wakulima kutotegemea zao moja bali
wajikite pia kwenye mazao mengine na kuwataka kampuni ya wanunuzi
kununua shahiri kwa wakulima wote .
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi.Theresia Mahongo amesema zao hili ni zao la
kibiashara linalowaingizia uchumi wakulima hivyo ametoa rai kwa
wanunuzi kuongeza tani kwa zao la shahiri kwani wakulima wanalima zaidi
ya tani 8,000 zinazohitajika
Mkurugenzi
wa Tanzania Bruweries (TBL) Bw.Philip Redman amesema kwa msimu ujao wa
2021,wameingia mkataba na wakulima 300 na kiwanda kina uwezo wa kuchukua
tani 5,000 kwa mwaka.
Kwa
upande wa Serengeti Breweries (SBL) Mkurugenzi wa Mahusiano Bw.John
Wanyancha amesema kuwa kwa msimu ujao wanatarajia kuchukua tani 3,000
kwa wakulima 60.
No comments :
Post a Comment