Mkurugenzi wa udhibiti Ubora wa
Shirika la Viwango Tanzania TBS, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza na
Wanahabari katika Ofisi za shirika hilo Jijini Dar es Salaam leo.
*************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Takwimu za Shirika la Afya Duniani
(WHO) juu ya makadirio ya tatizo la magonjwa yatokanayo na chakula
kisicho salama zilitolewa mwaka 2015 zinaonesha kuwa mtu 1 kati ya
10
duniani huugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama na
husababisha vifo vya watu takribani 420,000
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa
udhibiti Ubora TBS, Bw.Lazaro Msasalaga katika kikao cha waandishi wa
habari kilichofanyika katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
“Magonjwa haya yameripotiwa
kuathiri zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka 5,ambapo inakadiriwa
kusababisha vifo takribani 125,000 kila mwaka”. Amesema Bw.Msasalaga.
Pamoja na hayo Bw.Msasalaga
amesema takwimu hizo zinaonesha kuwa tatizo hilo ni kubwa zaidi katika
bara la Afrika, ambapo inakadiriwa watu zaidi Milioni 9 huugua na
137,000 kufa kila mwaka.
Aidha, amesema kuwa kwa hapa
nchini madhara mbalimbali yanayohusishwa na ulaji wa chakula kisicho
salama yamekuwa yakiripotiwa katika matukio mbalimbali.
“Magonjwa yatokanayo na chakula
kisicho salama yanaweza kuzuilika iwapo kila mmoja wetu atatekeleza
wajibu wake katika mnyororo wa chakula”. Amesema Bw.Msasalaga.
Bw.Msaalaga amesema kwa kutambua
umuhimu wa chakula salama,TBS imeweka mifumo ya kiudhibiti ili
kuhakikisha chakula kilichopo katika soko hapa nchini ni salama ili
kulinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na kula chakula kisicho
salama.
No comments :
Post a Comment