Naibu waziri wa Tamisemi Mhe.
Josephat Kandege akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Daniel Chongolo, Katibu Tawala Bi Stella Msofe pamoja na Mganga Mkuu
Dokta Samweli Laizer wakati akikagua upanuzi wa Zahanati ya Bunju
iliyopo katika Halmashauri hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Daniel Chongolo akimuonesha Naibu Waziri wa Tamiseni Mhe. Josephat
Kandege ujenzi wa mfereji wa kupitisha maji, mwenyeshati jeupe ni Meneja
wa TATURA Leopord Runji.
Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe.
Josephat Kandege akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pamoja na
wakandarasi wanaojenga barabara ya Shekilango Bamaga wakati wa ukaguzi
wa ujenzi wa barabara hiyo.
Muonekano wa ujenzi wa mfereji wa kupitisha maji.
Meneja wa TATURA Leopord Runji
akimuonesha Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Josephat Kandege hatua
inayoendelea katika ujenzi wa mfereji wa kupitisha maji.
Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe.
Josephat Kandege pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe.Daniel
Chongolo wakiangalia karavati za kuweka kwenye mifereji ya kupitisha
maji.
…………………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
Josephat Kandege ameridhishwa na matumizi ya fedha za mapato ya ndani ya
Halmashauri zilizotumika katika utekelezaji wa miradi ya maedeleo
iliyokamilika kwa wakati na
viwango.
Amesema kuwa
Manispaa hiyo ni mfano wakuigwa kwa kuwa imeonesha nidhamu nzuri katika
matumizi ya fedha zinazotokana na vyanzo vya mapato ya ndani na kwamba
miradi ambayo imetekelezwa kupitia fedha hizo inaendana na thamani
halisia.
“Kimsingi leo
nimemaliza ziara yangu katika Halmashauri hii, na kikubwa nilikuwa
nimelenga zaidi kuona fedha zinazokusanywa na Halmashauri na namna
ambavyo zinatumika katika miradi ambayo inaonekana na kimsingi naomba
niwapongeze sana Kinondoni, mnazitendea haki fedha zenu mnazokusanya”
amesema Mhe. Kandege.
Kadhalika Mhe.
Kandege ameridhishwa na kiwango cha barabara zinazojengwa katika
Halmashauri hiyo kupitia mradi wa DMDP na kusema kuwa kukamilika kwake
kutaleta mafanikio makubwa kwa wananchi hususani watumiaji wa barabara
ya Shekilango na kwamba itaondoa msongamano wa daladala na kuwawezesha
wananchi kuondokana na adha ya foleni.
Amefafanua kuwa
Mafanikio haya yanayoonekana leo Kinondoni ni kutokana na uongozi imara
wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli
pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi ndg. Aron Kagurumjuli ulioleta
tija kwa Wananchi.
Katika hatua
nyingine Mhe.Kandege ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kujenga kituo
cha Afya katika Kata ya Kigogo na kusema kuwa walifanya mamuzi ya
busara na yakujali wananchi kwakuwa eneo hilo halikuwa na Hospitali na
kwamba litawasaidia wakazi hao kupata huduma bora ya afya.
“Kinondoni
mliona mbali kuweka kituo cha Afya pale Kigogo, mlitumia busara ya hali
ya juu mkaona ni bora mnunue eneo kwa ajili ya kuwajengea wananchi kituo
cha Afya, hivyo hata kwenye Kata ya Kawe kwa ujumla ukiondoa Kawe kama
Kawe eneo lililobaki halikuwa na kituo cha Afya, pamoja na ujenzi wa
Hopsitali ya Wilaya nilazima uwe navituo hivi ili hata mgonjwa wa eneo
jirani apate huduma.
Katika ziara hiyo
Mhe. Kandege ametembelea Barabara ya shekilango inayojengwa kwa kiwango
cha lami kwa shilingi Bilioni 14. 8, mfereji wa Kilongawima uliyopo
Jimbo la Kawe kwa shilingi Bilioni 3.1 pamoja na upanuzi wa Zahanati ya
Bunju mradi unajongekwa cha shilingi Milioni 600.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Mahusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
No comments :
Post a Comment