Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nyasa, wawakilishi wa Serikali ya Kijiji na Polisi wa upande wa Msumbiji walropo mpakani hapo
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro (Mb) anaendelea na ziara ya siku sita (6) katika maeneo
ya mipaka iliyopo mkoani Ruvuma. Mpaka sasa Dkt. Ndumbaro amefanya
ziara katika mpaka wa Wenje uliopo Wilayani Tunduru, Chiwindi uliopo
Wilayani Nyasa na mpaka wa Magazini uliopo Wilayani Namtumbo Mkoa wa
Ruvuma. Mipaka hii inaiunganisha Tanzania na Nchi jirani ya Msumbuji.
Ziara
hii ambayo inatokana na utekelezaji wa majukumu ya Wizara, ikiwemo
utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ,kujenga, kulinda na kudumisha
uhusiano wa kimataifa, inalenga kuwahimiza watendaji na Mamlaka
mbalimbali za Mkoa na Wilaya za Mipakani kuhusu umuhimu wa wakudumisha,
kulinda, na kuendeleza uhusiano mzuri baina ya Taifa letu na nchi tunazo
pakana nazo ili kustawisha biashara baina yetu na nchi tunazopakana
nazo. Kadhalika, ziara hii inalenga kuhimiza umuhimu wa kulinda mipaka
ya nchi na kubaini changamoto zinazowakabili wakazi wa mipakani.
Aidha,
kwa upande wake Dkt. Ndumbaro amewataka watendaji na Wakuu wa Wilaya
hizo, kuendelea kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila
siku, vilele kutengeneza na kuanzisha masoko ya bidhaa mbalimbali
maeneo ya karibu na mipakani kwa lengo la kuchagiza biashara, ajira na
kuongeza mapato ya Serikali. “Wizara tumejipanga kutekeleza mkakati wa kuhakikisha kuwa tunashiriana kwa ukaribu na wadau wanaosaidia kutekeleza majukumu ya Wizara zikiwemo Mamlaka za Mikoa na Wilaya ambazo zipo mipakani” alisema Dkt. Ndumbaro
Wakati
huo huo katika ziara hii Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo
na kamati za ulinzi na usalama katika Wilaya ya Namtumbo ikiongozwa na
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Mhe Sophia Mfaume, Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tunduru ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya
hiyo Mhe.Julius Mtatiro na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Nayasa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Isabela Chilumba. Wakuu wa
Wilaya zote tatu pamoja Wakuu vya Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa
Wilaya hizo kwa nyakati tofauti waliambatana na Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro
kuzuru maeneo ya Mipakani.
Wananchi
wa Tunduru kwa upande wao wameishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mshariki kupitia Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro, kwa
kuwatembelea na kusikiliza changamoto zinazo wakabili. Baadhi ya
changamoto walizozitaja ni pamoja na kutokuwepo kwa huduma ya kivuko cha
uhakika, barabara (kiwango cha lami) ukosefu wa huduma ya maji safi na
salama ya uhakika na umeme. Hata hivyo Dkt. Ndumbaro ameeleza hatua
mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinatatuliwa.Aidha, Wananchi wa Chiwindi, Wilayani Nyasa wamemwomba Dkt. Ndumbaro kufikisha salaam na shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,
kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ya kuleta maendeleo nchini, na
hasa kwa kuzingatia mahitaji ya watu wa kipato cha chini.
Dkt.
Ndumbaro amezipongeza Mamlaka zilipo katika maeneo ya mipaka hiyo kwa
kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ya kulinda mipaka, kudumisha mahusiano
na nchi jirani na kwa kutekeleza kwa ufasaha dhana ya Diplomasia ya
Uchumi licha ya changamoto zinazowakabili. | | . | | |
No comments :
Post a Comment