Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama picha yake iliyochorwa na Tabibu wa Meno wa Kituo cha Afya cha
Kingorwila Morogoro, Sanjame Kayoka (kulia) wakati alipohutubia mkutano
wa hadhara katika Kata ya Nachingwea,Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea picha yake iliyochorwa na Tabibu wa Meno wa Kituo cha Afya cha
Kingorwila Morogoro, Sanjame Kayoka (kulia) wakati alipohutubia mkutano
wa hadhara katika Kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama picha yake iliyochorwa na Tabibu wa Meno wa Kituo cha Afya cha
Kingorwila Morogoro, Sanjame Kayoka wakati alipohutubia mkutano wa
hadhara katika Kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifurahia wimbo kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Sengeli, Hassan
maarufu kwa jina la Dogo H. wakati alipohutubia mkutano wa hadhara
katika Kata ya Nachingwea, Wilayani Ruangwa Juni 24, 2020.
Mwimbaji wa nyimbo za Sengeli,
Hassan marufu kwa jina la Dogo H akitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Nachingwea,
Wilayani Ruangwa, Juni 24, 2020. (
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………………………………………
*Awataka wakulima waendelee na kilimo katika kipindi hiki cha mpito
WAZIRI MKUU,
Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa mazao mbalimbali ya biashara
wakiwemo wakulima wa ufuta nchini waendelee na kilimo na kwamba suala la
kushukuka kwa
bei lililotokea kwenye msimu wa mwaka huu lisiwakatishe
tamaa kwani jambo hilo litakwisha.
Amesema
Serikali inaendelea kulifanyia kazi hilo na kwamba bei ya mazao nchini
itaimarika baada ya kuongezeka kwa ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao
nchini, ambapo wakulima watakuwa na masoko na uhakika na pia nchi
itauza bidhaa zitokanazo na mazao hayo na si malighafi.
Waziri Mkuu
alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Juni 24, 2020) wakati
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Lindi alipokuwa katika ziara ya
kikazina aliwasihi wakulima kutoacha kulima.
“Kushuka kwa
bei ya ufuta kusiwakatishe tamaa na kuwafanya muache kulima kwa sababu
bei haijashuka kwa zao hilo tu bali na mazao mengine kama chai, tumbaku,
kahawa, chai na mazao mengine. Hali hii imetokana na mlipuko wa ugonjwa
wa COVID-19 ambao umeikumba dunia.”
Waziri Mkuu
aliongeza kuwa Serikali inatarajia kwamba kadiri ugonjwa wa COVID-19
unavyoendelea kupungua katika Mataifa mbalimbali duniani hali bei ya
mazao nayo itaimarika, hivyo wakulima waendelee kuwa na subira katika
kipindi hiki ambacho ni cha mpito.
Waziri Mkuu
alitumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi
waje wawekeze katika viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali kwa sababu
watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi pamoja na nishati ya
kutosha.
Alisema moja
ya msisitizo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli ni kuboresha sekta ya kilimo ili iweze kujitosheleza kwa
chakula. “Suala la bei ya mazao linapangwa na wanunuzi Serikali
inasimamia tu.”
Pia, Waziri
Mkuu ameendelea kuwashukuru wananchi wa wilaya hiyo kwa umoja na
mshikamano mkubwa waliompatia katika kipindi chote cha miaka mitano na
amewasisitiza waendelee na ushirikiano huo kwa ajili ya maendeleo ya
wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment