…………………………………………………………………………….
Na WAMJW – Tanga
Serikali kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo wanaendelea kuboresha huduma za afya nchini ambapo
shilingi milioni 780 zimetolewa kwa ajili ya kujenga kliniki ya huduma
za
methadone kwa waathirika wa madawa ya kulevya mkoani Tanga.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya
Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa
uzinduzi wa kituo cha muda cha kutoa tiba ya methadone kwa warahibu wa
madawa ya kulevya kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –
Bombo.
“Kwa kushirikiana na wadau wetu wa
maendeleo Mfuko wa Dunia (Global Fund) na Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa
ya Kulevya tumepata zaidi ya milioni 780 na tumezileta kwa ajili ya
kujenga jengo la kutolea huduma ya methadone” amesema Waziri Ummy.
Hata hivyo waziri ummy mwalimu
hakusita kuupongeza uongozi wa mkoa wa tanga kwa ubunifu walioufanya kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo PEPFAR na Amref -Tanzania,
kwa kujenga kituo cha muda kwa ajili ya kutoa tiba kwa warahibu wa
madawa ya kulevya ambacho kimegharibu shilingi milioni 20 za Kitanzania.
“Tumeona tunaweza kufanya huduma
hizi kwa gharama nafuu, nnafurahi kuona kwamba zimetumika takribani
shilingi milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza kituo cha muda kwa huduma
za kliniki katika Mkoa wa Tanga” amesema Waziri Ummy.
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa
ilikuwepo haja ya kuwa na kliniki ya methadone kwa Mkoa wa Tanga
kutokana na kuwa na waathirika wengi wanaotumia madawa ya kulevya huku
mkoa huo ukishika nafasi ya pili ya kuwa nawarahibu wengi wa madawa ya
kulevya.
“Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya
pili ya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa madawa ya kulevya, takwimu
za mwaka 2016 zinaonyesha Mkoa wa Tanga una watumiaji taribani 5190 wa
madawa ya kulevya” amefafanua Waziri Ummy Mwalimu
Waziri Ummy amesema kuwa hadi sasa
kuna kiliniki 8 ambazo zinatoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini
ambapo kwa Mkoa Wa Dar Es Salaam kliniki hizo zimeanzia katika hospitali
ngazi ya mikoa na kushuka chini kwenye hospitali za ngazi ya
halmashauri na kutaja maeneo yatakayofuata kuwa na huduma hizo ni pamoja
na Bagamoyo, Kigamboni, Mbagala, Tegeta pamoja na Magereza Segerea.
Amesema kwa mujibu wa Takwimu za
Wizara ya Afya, Tanzania ina waathirika 8071 waoapatiwa huduma ya dawa
za methadone kwa ajili ya kupunguza madhara ya dwa za kulevya ambapo
kati yao wagonjwa 480 ni wanawake na 7591 ni wanaume.
Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka
ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya Bw. James Kaji amesema kuwa wiki hii
Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya kupinga madawa
ya kulevya ambayo kwa mwaka huu kauli mbinu ni tujenge uelewa sahihi
kwa tatizo la dawa za kulevya ili kuimarisha mapambano dhidi ya tatizo
hilo.
“Uzinduzi wa kituo hiki ni
muendelezo wa vituo vingine 8 vinavyotoa huduma nchini ambapo kwa Dar es
Salaam vipo vitatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya
Rufaa ya Mwananyamala na Temeke; Mbeya – Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za
Juu Kusini; Mwanza – Hospitlai ya Rufaa ya Sekou Toure; Bagamoyo na
Dodoma – Itega” amefafanua Kamishna Jenerali James Kaji
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Mhe. Martin Shigela amesema kuwa MKoa wa Tanga ni miongoni mwa
mikoa yenye idadi kubwa ya shughuli za usafirishaji wa madawa ya kulevya
na kufanya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji ambao hiingia kwenye
urahibu wa madawa hayo.
Aidha Mhe. Shigela ameiasa jamii
kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya huku akiwaomba kutoa taarifa
kwa mamlaka kwa wale wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya
madawa ya kulevya.
“Kwa wale ambao wameathirika na
madawa ya kulevya katika jamii zetu tuwaone ni kama sehemu ya ndugu
zetu, tusiwanyanyapae, tuwaelekeze na tuwalete kwenye matibabu na
tunaamini watarudi kwenye hali ya kawaida” amesisitiza Mhe. Shigela
No comments :
Post a Comment