…………………………………………………………………………
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Ndugu
Gerald M. Kusaya anawatangazia wanachuo na wakufunzi kuwa Vyuo vya
Mafunzo ya Kilimo (MATI) vimefunguliwa rasmi tarehe 01 Juni, 2020
kufuatia agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilotoa tarehe 21
Mei, 2020.
Wanafunzi wote wa Vyuo vya
Mafunzo ya Kilimo nchini wanatakiwa kuendelea kuripoti
vyuoni kwa ajili
ya kuendelea na masomo yao. Wizara inawataka wanafunzi wote kuhakikisha
wanakuwepo vyuoni ifikiapo tarehe 08 Juni, 2020 na itakapofika tarehe 10
Juni, 2020 Wakuu wa Vyuo vyote wachukue hatua za kinidhamu na kitaaluma
kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajaripoti vyuoni. Aidha, Wakuu wa Vyuo
vyote vya Kilimo wanatakiwa wafanye maboresho ya kalenda ya masomo kwa
kuzingatia maagizo ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
yaliyotolewa tarehe 22 Mei, 2020
Wizara ya Kilimo inasisitiza
kuwa watumishi na wanafunzi wote vyuoni waendelee kuzingatia kanuni zote
za kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19) kama
zilivyotolewa katika mwongozo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
Katika hatua nyingine, Katibu
Mkuu ameelekeza wazabuni wote wanaotoa huduma ya chakula vyuoni,
waendelee kutoa huduma hiyo ili kuhakikisha chakula kinapatikana muda
ambao wanafunzi watakuwa wakiendelea na masomo yao.
No comments :
Post a Comment