Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu
kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo amepokea msaada wa
hundi ya kiasi cha Tsh. Milioni 100 kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma
za Nishati na Maji (EWURA)uliokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Bw. Godfrey
Chibulunje akiwa na Meneja Mawasiliano na uhusiano wa mamlaka hiyo Bw.
Titus Kaguo kulia.
Aidha, Waziri Ummy amepokea
msaada wa ndoo 480 sawa na Lita 9600 za vitakasa mikono (Hand Sanitizer)
zenye thamani ya Tsh. Milioni 11 zilizotolewa na kampuni ya Mafuta ya
Mount Meru ambazo zitatumika katika kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini.
Vitakasa mikono hivyo vimekabidhiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw.
Prabhat Yadau.
Katika makabidhiano hayo
yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma, Waziri
Ummy kwa niaba ya Waziri Mkuu ameshukuru kupata misaada hiyo ambayo
itasaidia katika kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini na pia amewataka
wananchi kuendelea kuchukua tahadhari licha ya maambukizi ya ugonjwa huo
kupungua nchini.
No comments :
Post a Comment