Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo akisisitiza Jambo wakati akiongea na Maafisa na Askari wa
Polisi Kata Mkoa wa Arusha katika kikao kazi cha kukumbushana wajibu wa
Polisi kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Kikao hicho kimefanyika
katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Arusha leo tarehe
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
ACP Jonathan Shanna akiongea na Maafisa na Askari wa Polisi Kata Mkoa wa
Arusha katika kikao kazi cha kukumbushana wajibu wa Polisi kabla,
wakati na baada ya uchaguzi. Kikao hicho kimefanyika katika Bwalo la
Maafisa wa Polisi Arusha leo
Wakuu wa Polisi toka Wilaya zote
Saba za Mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo wakati akizungumza na Maafisa na Askari Kata katika kikao kazi cha
kukumbushana wajibu wa Polisi kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Kikao
hicho kimefanyika katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Arusha
Waratibu Tarafa na Askari Kata 157 toka kata zote za Mkoa wa Arusha walioshiriki katika kikao kazi cha kukumbushana wajibu wa Polisi kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Kikao hicho kimefanyika katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Arusha leo
…………………………………………………………………
Na Gasto Kwirini wa Jeshi la Polisi Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa
kufanikiwa
kupunguza na kudhibiti matukio ya uhalifu hali ambayo imepelekea
shughuli za kiuchumi kufanyika kwa amani hasa utalii.
Alitoa pongezi hizo wakati
akifungua kikao kazi kilichohusisha Maafisa wa Polisi pamoja na Polisi
Kata 157 toka kata zote za Mkoa wa Arusha ambacho kilikua na lengo la
kukumbushana wajibu wa Polisi Kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Amesema kuwa kupitia Jeshi la
Polisi, Mkoa wa Arusha kwa sasa matukio makubwa ya uhalifu yamepungua
kwa kiasi kikubwa huku akitolea mfano mauaji na kubakwa kwa wanawake
katika kata ya Olasiti ambapo kwa sasa matukio hayo yamedhibitiwa.
‘‘Jana nimefanya ziara katika
kata Olasiti, kata ambayo ilikuwa inasumbua sana kwa mauaji ya akina
Mama, jana wametoa pongezi wakasema sasa tunalala, akina mama wanatembea
masaa 24 kifua mbele kwa sababu ya uwepo wa Jeshi la Polisi’’. Alisema
Gambo
Aidha aliwataka Maofisa pamoja
na Askari hao kuhakikisha uchaguzi Mkuu ujao unafanyika kwa amani na
utulivu. Pia alisisitiza mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu
yaendelee ili Mkoa uendelee kuwa shwari wakati wote.
Awali akimkaribisha Mkuu wa
Mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Jonathan Shanna alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoani hapa litaendelea
kufanya kazi kwa weledi na nidhamu kuhakikisha matukio yote ya kihalifu
yanadhibitiwa.
Aliongeza kwa kusema
watahakikisha uchaguzi ujao unafanyika kwa amani na utulivu bila kutumia
nguvu kubwa hasa mabomu ya machozi na silaha za moto badala yake
litahakikisha linalinda amani kwa raia.
Aliwataka Wanasiasa na
Wananchi kufanya siasa za kistaarabu, na kwa wale wachache ambao hupenda
kuvuruga amani wakati wa uchaguzi kuacha fikra hizo kwani watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Katika Kikao hicho Askari hao
walipata fursa ya kufundishwa mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Ugunduzi na Upelelezi wa Makosa ya Uchaguzi, ushirikishwaji wa jamii
katika kufanikisha uchaguzi, elimu juu ya haki za raia katika uchaguzi
na utayari wa Jeshi la Polisi katika kipindi chote kabla, wakati na
baada ya uchaguzi.
No comments :
Post a Comment