Mhe.Shamillah Sarwatt, akifafanua jambo kuhusu mabadiliko hayo.
……………………………………………………………………………………
NA INNOCENT KANSHA – Mahakama
Mahakama ya
Tanzania imefanya Maboresho na inaendelea kufanya maboresho katika
maeneo yote muhimu ya utendaji kazi kupita nguzo tatu za Mpango Mkakati
wa Miaka Mitano ulioanza kutekelezwa mwaka 2015/16 hadi mwaka 2019/20.
Nguzo hizo ni
Utawala, Uwajibikaji na Matumizi ya Bora ya Rasilimali, Upatikanaji wa
haki sawa kwa wote na kwa wakati na Kujenga taswira chanya na Kurejesha
imani ya wananchi kwa Mahakama.
Hivyo maboresho
ya sheria na kanuni mbalimbali yaliyofanywa na Mahakama ya Tanzania
katika kurahisisha utoaji wa haki maana yake ni kuhakikisha sheria zile
ambazo hazikuwa rafiki zilikuwa na muonekano wa utaratibu wa zamani
basi kuwekewa utaratibu mpya unaoendana na hali ya sasa.
Kwa upande wa
kanuni kama zilikuwa na utaratibu ambao sasa umepitwa na wakati basi
kupitia Maktaba Kuu ya Mahakama ya Tanzania, hupokea majuzuu ya sheria
hizo kwa kushirikiana na Katibu wa Kamati ya Sheria/Kanuni, ambayo
huweza kushauri sheria zipi na kanuni zipi ambazo ni za zamani
zinazohitaji kuboreshwa.
Maboresho
yanafanyika pale ambapo kamati hiyo inaona kwamba sheria za sasa,
katika muda huu hazifai kutumika na ni vitu gani vinafaa kutumika.
Akizungumzia
kuhusu maboresho hayo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maktaba Mahakama ya
Tanzania Mhe. Kifungo Mrisho , ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo
alisema ‘‘Katibu wa Kamati ya Sheria na Kanuni huchukua kile ambacho
huonekana ni bora na kuhakikisha kwamba kanuni/sheria hizo zinafika kwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni/Sheria. Mwenyekiti huyo huchaguliwa na
Jaji Mkuu akipata mawazo yoyote kuhusu maboresho ya sheria/kanuni
huwasiliana na Jaji Mkuu ili kuitisha kamati kupitia sheria hizo na
kuweka maboresho hayo kama ni ya sheria au kanuni”.
Kamati hiyo
inakuwa na utaratibu wa kuchukua maoni hayo ambayo yamekamilika na
sheria hizo ambazo zimefanyiwa mabadiliko na kuwasilisha kwa Jaji Mkuu,
ambaye ana uwezo wa kuhakikisha kwamba sheria na kanuni hizo ambazo
zimefanyiwa marekebisho zinapelekwa kwa wadau, ambao ni wahe. Majaji,
Wasajili, Mahakimu na Mawakili wa kujitegemea kwa ajili ya kuleta maoni
yao.
Mrisho aliongeza
maoni hayo yakishaletwa kamati hiyo hukaa vikao kwa ajili ya kuyaangalia
na kuweza kutunga sheria/kanuni iliyokamili ili kuja na sheria/kanuni
iliyokamili kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maboresho yamefanyika
kuendana na wakati.
‘‘Kwa kifupi tu,
ni kwamba Mhe. Jaji Mkuu kupitia Sheria Sura Namba 354 Judicature and
Application of laws Act (JALA) sheria hii humpa mamlaka ya kutengeneza
kanuni za Mahakama Kuu, lakini pia katika sheria yoyote ile inayotungwa
na Bunge, hata hivyo kuna zinazompa mamlaka Waziri kutengeneza kanuni
au taratibu za kimuongozo wa namna gani sheria husika itumike lakini
kuna sheria zingine zinazompa mamlaka Jaji Mkuu kutengeneza kanuni au
taratibu .
Akitolea
ufafanuzi wa taratibu za maboresho alisema pale ambapo Jaji Mkuu amepewa
mamlaka ya kutengeneza sheria fulani au kanuni kupitia kamati yake
ikishaona hilo, kwa mfano, Sheria ya Vyombo vya Habari iliyotungwa mwaka
2017 (Media Service Act of 2017) Mhe. Jaji Mkuu alipaswa kutengeneza
kanuni. ‘‘Hivyo kamati hiI hungalia zile sheria zinazotakiwa kutungiwa
kanuni na kumshauri , Jaji Mkuu ambaye hutoa agizo kwa kamati sasa
kanuni zitengenezwe”.alisisitiza.
Alisema hata
kama kuna sheria yoyote ya mabadiliko inayohitaji maboresho
yanayofanyika bungeni au labda inataka kwenda bungeni bado kamati hiyo
hushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha kwamba
ile sheria ambayo inakuja basi iwe na ahuweni katika ubora kwa ajili ya
kuendeshwa katika Mahakama na misingi mizuri ya upatikanaji wa haki.
“Hata mwaka 2016
kamati ya kanuni iliweza kupendekeza mabadiliko ya Sheria Sura Namba
141 ambayo ni Sheria ya Rufani inayotoa mamlaka ya kusajili rufaa katika
Mahakama ya Rufani Tanzania haikuwa na kipengele cha mapitio (review)
lakini kamati ya kanuni iliweza kushauri kufanyika maboresho hayo”
alisema Mrisho.
Mabadiliko ya
Kanuni za Mahakama ya Rufani Tanzania ya 2019 (The Tanzania Court of
Appeal Rules) yameleta kanuni za utendaji haki, bila kuzingatia taratibu
za kiufundi zilizopitiliza (overriding objectives).
Kanuni hizi
zinajulikana Kama “oxygen principle” Kama zinavyoainishwa chini ya
kifungu cha 3A na 3B cha Sheria ya Mamlaka ya Mahakama ya Rufani
Tanzania (The Appellate Jurisdiction Act). Kanuni hizi zinaitaka
Mahakama kuepuka taratibu za kiufundi katika kufikia utoaji wa haki.
Kuanzia mwaka
2016, 2017, 2018 na 2019 kuna mabadiliko ya maboresho ya kanuni mengi
yamekwishafanyika na yapo kwenye matumizi lakini ni mabadiliko
yanayoletwa na maboresho ya sheria zinazotumika mahakamani kwa kupitia
kamati hiyo.
Alifafanua kuwa
hadi sasa sheria na kanuni , ambazo zimekwisha pitishwa na kutangazwa
kwenye gazeti la Serikali ni kanuni 41, lakini mapendekezo mengi
yamekwisha fanyiwa kazi na kamati ya maboresho, pia takribani sheria 38
zimefanyiwa kazi ingawa hazitangazwa katika gazeti hilo.
Lengo likiwa ni
kurahisiha utaratibu mzima wa uendeshaji wa mashauri kuanzia hatua ya
awali ya upokelewaji wa shauri hadi hatua ya mwisho kabisa ya
utekelezaji wa tuzo uliotokana na hukumu au uamuzi ama amri ya Mahakama.
Mrisho alisema
kuwa ikumbukwe kamati hiyo ilianzishwa Julai, mwaka 2014 wakati wa
utawala wa Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Othuman Chande na Mwenyekiti wake wa
kwanza alikuwa Mhe. Jaji Edward Rutakangwa kamati inaundwa na Wahe.
Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wanne, Wahe. Majaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania wanne na pia sekretarieti ya wataalamu watatu ambao
wote ni wanasheria wabobezi.
Hadi mwaka 2019
wakati kamati hiyo ilifanya kazi ya mwisho ya kupitisha utaratibu wa
kuweza kutoa hukumu au kutoa adhabu kwa mahakimu (Sentencing Guideline
Manual) ambao umepitishwa Desemba, mwaka 2019, na Kamati ya Maboresho ya
Kanuni na kuzinduliwa. Januari 31, mwaka 2020.
Hizi zote ni
taratibu ambazo zinazoboresha ufanisi wa kazi wa Mahakama, utaratibu huu
umewekwa kisheria ufuatwe ili kuongeza tija katika utendaji wa kazi.
“Kamati hii
inashughulikia mambo mengi kama vile kutoa mapendekezo juu ya utoaji wa
vitabu mbalimbali vya maelekezo au miongozo mfano kamati inatoa ushauri
juu utoaji wa kitabu cha maelekezo au mwongozo wa ukazaji wa hukumu
(Execution Guideline Manual), pia kuna mwongozo mwingine wa watumiaji wa
Mahakama ili kuwapa uelewa mpana watumiaji kujua taratibu za
Mahakama.(Court users Guideline Manual)” alisema.
Kingine cha
Mwongozo wa Usimamizi wa Mashauri (Case Management Guideline) hii
inasaidia taratibu za uendeshaji wa kesi mahakamani, kitaelezea taratibu
za uendeshaji wa kesi mbalimbali kama vile madai, jinai, talaka,
mirathi na kesi nyingine nyingi zinazofunguliwa mahakamani.
Kwa upande wake
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Shamillah Sarwatt,
alisema maboresho haya yametoa mwanga chanya kwa Mahakama na wadau
mfano; Kanuni za Kusajili kesi kwa njia ya Mtandao (Electronic Filing
Rules) za mwaka 2018.
‘‘Zinatoa fursa
kwa Wakili wa Serikali na wa kujitegemea ama mtu mwingine yeyote
kusajili shauri mahala popote pale alipo bila kulazimika kufika
mahakamani kwa kutumia Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
vivyo hivyo kwa kutumia kanuni hizi mlolongo wa taratibu nzima za
usajili wa mashauri umerahisishwa na hivi sasa inachukua siku moja tu
badala ya hapo awali ilikuwa inachukua muda mrefu zaidi,”alisema.
Msajili huyo.
Sarwatt
aliongeza kuwa mabadiliko mengine yaliyofanyika ni ya Sheria Anuai
Namba 8 ya Mwaka 2018 ambayo imefanyiwa marekebisho, ikiwemo Sheria ya
Mamlaka ya Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyoiwezesha Mahakama hiyo,
kutofungwa na sababu za kiufundi wakati wa kusikiliza shauri.
Nyingine ni
Sheria ya Migogoro ya Ardhi Sura Namba 216 kama ilivyofanyiwa marejeo
mwaka 2002 (Land Dispute Act Cap. 216 RE 2002) nayo imefanyiwa
marekebisho na kuruhusu Wahe. Mahakimu wenye mamlaka ya nyongeza
kusikiliza mashauri ya migogoro ya ardhi katika Mahakama Kuu ya
Tanzania.
Kupitia maboresho
kuna mabadiliko ya jedwali la sheria za madai na taratibu zake ya mwaka
2019, yamepunguza hatua za usikilizwaji wa mashauri ya madai kutoka
hatua 38 hadi hatua 22 tu zitakazo tumika mahakamani.
Maboresho haya
lengo lake ni kusaidia uharakishwaji wa utoaji wa haki kwa wakati na kwa
wote, urahisishaji wa utaratibu mzima wa kuendesha mashauri unalenga
katika kupunguza muda wa shauri kukaa mahakamani hivyo kutoa fursa kwa
mdaawa wa shauri kutumia muda huo katika shughuli za uzalishaji mali kwa
faida ya mtu mmoja mmoja na kwa Taifa letu kwa ujumla. Msajili wa
Mahakama Kuu ya Tanzania,
No comments :
Post a Comment