Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo (MATI) Ilonga, Abdallah Gulana akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) walipotembelea chuo hicho
kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro hivi karibuni.
Mratibu wa Masomo na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Felix Mrisho (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) walipotembelea chuo hicho hicho
kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro hivi karibuni.
Mkufunzi
na Msimamizi Mkuu wa Mashamba ya chuo hicho, John Ngairo (kulia) akitoa
maelezo kwa wanahabari kuhusu shamba la mpunga la chuo hicho ambalo
limelimwa kisasa.
Mahindi yakivunwa katika shamba la chuo hicho.
Msimamizi wa shamba la mifugo la chuo hicho, Elias Mkweso akizungumzia ufugaji bora wa nguruwe.
Ng’ombe wanaofugwa katika chuo hicho wakiwa malishoni.
Mkufunzi Hamisi Ramadhani wa Idara ya Chakula na Lishe, akizungumzia jinsi wanavyo sindika mazao ya kilimo chuoni hapo.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, Burton Nyasi akizungumzia faida ya masomo wanayopata chuoni hapo.
Mwanafunzi wa chuo hicho, Idara ya Mifugo, Keneth Komba akizungumzia ufugaji bora wa ng’ombe.
Msafara kuelekea kwenye miradi ya chuo hicho.
Shamba la migomba la chuo hicho.
Mratibu
wa Masomo na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Felix Mrisho (kulia),
akizungumzia teknolojia ya kilimo kwa kutumia kitalu nyumba
wanayoiendesha kwa kushirikiana na Shirika la Sustainable Agriculture
Tanzania (SAT).
Mkuu wa Idara ya Usindikaji chuoni hapo, Moses Chavala, akielezea namna wanavyotoa mafunzo ya usindikaji.
Wakufunzi
wa chuo hicho, Antoneta Sunguya na Mariam Marianda wakionesha sufuria
inayotumika kuchemshia nyanya kabla ya usindikaji.
Jengo la Utawala la chuo hicho.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utumishi Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Philbert Lutale, akiongoza moja ya vikao kazi chuoni hapo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utumishi Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Philbert Lutale, akiongoza moja ya vikao kazi chuoni hapo.
Baadhi ya Wakuu wa Idara wakiwa katika moja ya vikao kazi chuoni hapo.
Baadhi ya Wakuu wa Idara wakiwa katika moja ya vikao kazi chuoni hapo.
Mwanafunzi
wa chuo hicho, Noves Magomelo wa Idara ya Kilimo Hai kisichotumia
chemikali za viwandani cha mazao ya mbogamboga za majumbani akizungumzia
kilimo hicho.
Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Morogoro
CHUO cha Mafunzo ya Kilimo cha ‘Mati Ilonga’ kimezidi kupanua wigo kwenye
eneo la mafunzo ya uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, na sasa kipo mbioni kuboresha mfumo wake wauzalishaji mali ili kwenda sambamba na mahitaji ya soko.
Kaimu
Mkuu wa chuo hicho, Abdalah Gulana, alibainisha hayo wakati akizungumza
na waandishi wa Habari waliotembelea chuo hicho, kilichopo wilaya ya
Kilosa, mkoani Morogoro hivi karibuni.
“Shabaha
yetu kwa sasa ni kuboresha‘model’ ya uzalishaji ili kwenda sawia na
mahitaji yasoko. Msisitizo wetu mkubwa ukiwa ni kuanza kuzalisha kwa
kuzingatia tafiti zetu kuhusu mahitaji ya soko,” alisema Gulana.
Alisema
chuo hicho chenye uwezo wa kupokea zaidi ya wanafunzi 300 bado kina
fursa nyingi kwa tija na mabadiliko chanya kwenye eneo la uchumi wa
viwanda, huku akiomba serikali na wadau kutoa msukumo wa kipekee,
hususan kwenye rasilimali fedha kukiwezesha kupanga, kuandika,
kukarabati miundo mbinu na vifaa chakavu, sanjari na kuanzisha miradi
mipya kwa pamoja ili kukitegemeza.
Gulana
alisema kwa sasa wamejikita katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na
mifugo na hatima ye hatua ya usindikaji kupitia kiwanda kidogo
walichonacho kabla ya kupeleka bidhaa zao sokoni, huku nguvu kazi ya
uzalishaji husika ikifanywa na wanachuo kwa zaidi ya asilimia 50.
“Tunafundisha
wanafunzi ambao ni maafisa ugani tarajiwa na mfumo wa hapa Mati Ilonga
tunatumia zaidi vitendo kuliko na dharia, lengo letu hasa ni kuwawezesha
wahitimu kutoka na teknolojia stahiki kama wataalamu kwa tija na
ustawi wa taifa,” alisema.
Kaimu
Mkuu huyo ambaye pia ni mtaalamu kutoka idara ya elimu na ushauri kwa
wakulima chuoni hapo, aliyataka makundi mbalimbali, taasisi na mashirika
ndani ya jamii kuchangamkia fursa za kozi fupi za kati ya siku 3 mpaka 7
zinazotolewa chuoni ili kupata teknolojia mpya ambayo itawezesha
kuongeza tija kupitia mafunzo ya kilimo cha kisasa, na usindikaji wa
mazao ya kilimo na mifugo.
Alisema
kozi nyingine ndefu zinazofundishwa na chuo hicho ambacho kipo umbali
wa takribani kilometa 100 kutoka Morogoro mjini, na kilometa 10 toka
Kilosa mjini, ni pamoja na stashahada na astashahada kwenye maeneo ya
Usindikaji wa mazao kilimo na lishe, Sayansi ya Mifugo, Sayansi ya
Mimea, Zana za Kilimo na Mafunzo ya Wakulima na Huduma za Ugani.
Aidha,
Gulana mbali ya kuipongeza serikali kwa jitihada kadhaa za uboreshaji
wa vyuo vyake, aliomba changamoto kadhaa zilizopo chuoni hapo kupewa
msukumo wa kipekee, ikiwemo tatizo la uhaba na uchakavu wa vitendea kazi
na miundombinu muhimu ili kuleta tija na kuongeza kasi ya uwajibikaji.
Changamoto
nyingine ya chuo hicho kilichofunguliwa takribani miaka 48 iliyopita na
Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ni pamoja na kukabiliwa na uhaba wa
watumishi pamoja na rasilimali fedha katika kukiwezesha kutekeleza
majukumu yake kwa wakati.
“Tunampongeza
Rais Magufuli kwa kutilia mkazo uboreshaji wa kilimo kwa lengo la
kupata malighafi za viwanda ambavyo kwa sasa ndio injini ya kutufikisha
kwenye uchumi wa kati na kujitosheleza kwa chakula,” alisema Gulana.
Kwa
upande wake, Mratibu wa Masomo na Makamu Mkuu wa Chuo, Felix Mrisho
alisema chuo hicho chenye ukubwa wa eneo la ekari 595.5 sawa na hekta
237.8 ndoto yake ni kuwa taasisi bora inayotoa mafunzo ya uzalishaji na
usindikaji wa mazao ya kilimo.
Alipongeza
mashirika ambayo ni wadau wa maendeleo, wakiwemo SAT na JICA huku
akieleza mpango uliopo wa kuwa na kituo kikubwa cha biashara ambacho
kitatambulisha na kutumika kama soko la bidhaa zote zinazozalishwa
chuoni hapo.
“Tayari
tumeandika andiko na tumepeleka kwenye moja ya taasisi za elimu
tukiomba kusaidiwa fedha kwa ajili ya kuboresha idara nzima ya
usindikaji na ujenzi wa kituo cha biashara. Baada ya tathmini pamoja na
mambo mengine, chuo kiliamua kuongeza uzalishaji, kusindika kupitia
kiwanda chake kidogo na kupeleka bidhaa sokoni,” alisema Mrisho
No comments :
Post a Comment