*****************************
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma
Girres Muroto amethibitisha kushambuliwa na kujeruhiwa Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kiongozi wa
kambi ya
upinzani bungeni Freeman Mbowe usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake
jijini Dodoma.
Kamanda Muroto ameyasema leo
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma amesema kuwa
taarifa za tukio wamezipata majira ya saa moja asubuhi wakati tukio
limetokea usiku wa saa sita.
“Asubuhi ya leo nimepokea taarifa
kutoka kwa dereva wa Mbowe Wilhard Urasa kwamba wakati Mbowe alikuwa
anatoka eneo la Medeli kuelekea nyumbani kwake Area D ,baada ya
kushushwa kwenye gari wakati anapandisha kwenye ngazi kuelekea nyumbani
kwake,alikutana na watu watatu ambao hakuwafahamu kwa sura wala kwa
majina , walimkanyaga kwa mateke na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili
wake na kumvunja mguu wa Julia.”
Muroto amesema kuwa baada ya tukio
hilo Mhe.Mbowe alichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Ntyuka jijini
Dodoma ambako anaendelea na matibabu.
Kamanda Muroto amesema,jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa kina na kwamba hakuna kitu kitakachoachwa katika tukio hilo
Aidha ameonya kwamba tukio hilo lisitumike kisiasa kwa watu ama chama kujitafutia umaarufu.
Aidha ameonya kwamba tukio hilo lisitumike kisiasa kwa watu ama chama kujitafutia umaarufu.
“Bado tunafanya uchunguzi kujua
undani wa tukio maana eneo lile lina walinzi na majirani,hivyo
watahojiwa ili kujua ukweli.”amesema Muroto.
Ametumia nafasi hiyo kuwaonya
wanasiasa wanaopanga kufanya mikusanyiko isiyo halali huku akisema kwa
watakaofanya hivyo sheria itachukua mkondo wake.
“Tunaona kwenye mitandao ya
kijamii kwamba kuna baadhi ya watu wamepanga kukusanyika kwenye chama
cha chadema, jeshi la polisi lipo macho na yeyote atakayekusanyika
kichochezi atashughulikiwa.” Amesisitiza na kuongeza.
“Natoa onto kwa watu wanaotaka
kutumia tukio hili kama mtaji wa kisiasa,mitandao ya kijamii isitumike
vibaya kueneza uongo ,kwani wapo wwnaojiandaa kutumia tukio hili kufanya
machafuko,nawaonya waache Mara moja na wasiingilie kupotosha uchunguzi a
jeshi la polisi unaendelea ili ufalifanye kazi yake.”
Kwa upande wake Mnadhimu wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni Ester Bulaya amesema,uongozi wa Chadema
unapanga kumhamishia jijini Dar es salaam kwa matibabu zaidi na kwa
ajili ya usalama zaidi.
No comments :
Post a Comment